Hadithi zetu




ALICE THE SUPER STAR 43

Alijibu Larry na kuwafanya watu wote waliokuwepo hapo kwenye mkutano wacheke kasoro Deka ambaye alijisikia aibu na kuinama cnini.
“kidato cha nne?..............huwezi kumuoa mtoto wetu kwa kiwango hicho cha elimu. Kasome kwanza kijana ndio uje huku.... sawa?”
Baada ya kicheko cha muda mrefu kilichomfanya Larry ajisikie vibaya. Hatimaye kauli hiyo ilitoka kinywani mwa baba yake mzazi Deka.
Baada ya kikao kuisha. Larry aliaga na kuondoka.
Sis. Dka alimuwahi Larry air port kabla hajapanda ndege na kurudi nchini Tanzania.
“nakuomba Larry usiondoke.” aliongea Deka baada ya kumfikia Larry alipokua kwenye benchi.
“kwanini?... Naenda kusoma ili nije kukuoa... Si ndivyo baba yako alivyosema?... Mh... Eti una elimu gani... Naomba wafuate wenye madigree yao huko na si mimi Deka.” aliongea Larry na kumuangalia Sis. Deika kwa hasira.
“sio mimi lakini ambaye nilikua napenda hali kama ile itokee. Hata mimi imeniuma ndio maana nahitaji tuongee ili tufikie muafaka.” ali lalamika Deka.
“sikiliza Deka. Mimi nimeishi maisha ya kimasikini kabla ya haya ninayoishi sasa. Hivyo kama unajua masikini anavyochukia dharau, basi hata mimi nimekuchukia wewe na familia yako kwa dharau walizozionyesha juu yangu.” aliongea Lary na kuimtazama Deka kwa macho makali.
“let me go... Find  educated man”
Alimaliza hivyo Larry na kuondoka. Alimuacha Deka pale akilia na kuzihesabu hatua zake na kuondoka.

Kampuni ya ndege yeye makazi yake nchini Tanzania, ndio iliyombeba Larry akiwa na mawazo mengi tayari kwa kumrudisha nchini kwake.
Taratibu ndege ikapaa na Larry akaiaga ardhi ya south Africa na kurudi Tanzania.

Alifika na kufikia kwenye hoteli aipendayo kwanza kabla hajaenda nyumbani kwake.
Kutokana na uchovu aliokua nao. Alienda kuoga na kujilaza kitandani. Kabla hajapata usingizi, simu yake iliita na kumfanya Aipokee haraka bila kumuangalia ni nani apigaye.
“nahitaji mazungumzo na wewe Larry... Haiwezekani nikukose.” aliongea Deka na kumfanya Larry aiweke simu yake pembeni na yeye kugeukia upande wa pili wa kitanda. Hakuikata mpaka alipohakikisha kua Deka amekata simu. Ndipo alipoichukua simu yake na kuizima kabisa.

Siiku ya pili yake mchana, alienda kwenye kampuni ya Alice The Super star. Ilikua mshangao kwa kila mmoja ambaye alimuona Larry pale. Alimuulizia Director na kuonana nae.
“nimefurahi sana kukuona Larry. Ndio tulikua tunajiandaa kwenda nyumbani kwa kina Alice. Kuna sherehe kidogo inafanyika pale.” aliongea Director.
“sherehe?.... Ya nini?” aliuliz kwa mshangao Larry.
“Alice amesharejewa na fahamu. Hivyo wazazi wake wameamua kuandaa sherehe kwa tukio hilo.
“sawa.... Ila si dhani kama naweza kwenda. Ila mkipata nafasi ya kuzungumza na Alice, muambie kua nimemkumbuka sana.” aliongea Larry na kumuangalia Director ambaye alikua mnyonge wakati huo.
“twende bwana... Unajua hata wazazi wa Alice walikua na kinyongo kipindi hicho tu. Lakini hivi sasa wameshajirudi kutokana na mtoto wao kuwa na hali nzuri hivi sasa.” aliongea Director.
“nyie nendeni... Mimi sitoweza kuonana na Alice kwa muda huu.ila kama akihitaji kuonana na mimi, nipo free kwa ajili yake.” aliongea Larry na Director hakuona haja ya kumng`an`ganiza.
Waliagana na Larry akaondoka.

Baada  ya masaa mawili, walifika kwenye sherehe hiyo fupi na kusheherekea pamoja na Alice. Ilikua furaha tupu kwa mkurugenzi wao kurejea tena na nguvu zake kama awali. Hawakuacha kumuambia msaada walioupata kutoka kwa Larry mpaka kufikia pale ambapo kampuni yao imekua kwa asilimia thelathini toka Alice alipoiacha.
Ilikua na hisa nyingi kutoka kwenye makampuni makubwa na waliongeza pia biashara zingine zilizoiingizia kampuni hiyo mapato makubwa.

“isingekua hii sherehe inafanyikia nyumbi kwenu, tungeweza kumdanganya Larry ili  iwe suprise yako. Kutokana na kufanyika hii sherehe kwenu, amekataa kuja kwa kudai kuwa wazazi wako wanamchukia. Ila amesema kua yupo tayari kuonana na wewe kama ukihitaji.” aliongea Director baada ya sherehe hiyo kumalizika.
“anaishi wapi kwa hivi sasa?” aliuliza Alice.
“nyumbani kwake.. Pia ameniambia amebadilisha namba ya simu. Kwa sasa anatumia namba hii.” aliongea Director na kumfanya Alice aiandike ile namba haraka na kuihifadhi kwenye kitabu chake cha simu.
Baada ya wageni wote kuondoka. Alice alirudi chumbani kwake na kujifungia. Alilala kitandani na kumpigia simu Larry.
“haloo.”
Sauti ya Larry ilisikika masikioni mwake baada ya kuikosa kwa miezi kadhaa. Alifarijika sana japokua hakua na uhakika kama bado anaishi mwenyewe mpaka hivi sasa.
“haloo.” aliitikia Alice kiunynonge.
“habari yako Alice.”
Aliongea Larry kwakua alikua anaijua sauti ya Alice.
“safi.. Za kupotea ndugu yangu.” aliongea Alice na kumfanya Larry ashindwe kuongea kwa haraka. Alitulia sekunde kadhaa mpaka Alice aliposema haloo na kuangalia kama simu bado ipo hewani.
“sijapotea.. Ila napenda kutumia nafasi hii kukupa pole kwa maswahibu yote yaliyokukuta. Pole sana Alice.” aliongea Larry na kumfanya Alice atabasamu.
“nimeshapoa... Nawez kukuona kesho?” aliongea Alice na kumfanya Larry ajibu haraka.
“panga muda.. Mimi nipo free muda wote.” aliongea Larry na kumfanya Alice ataje muda ambao utakua mzuri kwao kuongea.

Walikubaliana wakutane nyumbani kwa Larry. Alice alifika na kuoana na Larry. Alikua kama mgeni kwa jinsi alivyokuta nyumba ya Larry ikiwa na ulinzi wa kutosha. Hakuwahi kufika zaidi ya kupasikia tu, ila alijiona kama vile ni malikia ambaye anaingia katika kasri la mfalme.
 Alifarijika sana baada ya kuona gari lake limepaki mlangoni anapotakiwa kuingia.
Alimkuta Larry akimsubiri kwenye sebula yake kubwa.
“karibu sana Alice.”
Aliongea Larry na kumuonyesha Alice sehemu ya kukaa.
“hongera sana Larry... Nimeamini kua wewe ni mpiganaji wa maisha.” aliongea Alice baada ya kuangaza macho yake na kujikuta amenogewa na sebule ya ya Larry.
“kawaida tu.. Niambie unatumia kinywaji gani?.”  aliuliza Larry na kwenda kuleta kinyaji anachokitumia Alice na kurudi tena sebuleni.
“nafahamu mimi ndio msababishaji wa ajali iliyokufanya usifanye shughuli zako kwa kipindi cha miezi nane. Naomba nisamehe kwa hilo.” aliongea Larry na kumuangalia Alice.
“usijali... Cha muhimu nimeshapona...... Vipi, kuna mtu unaishi nae humu ndani?” aliuliza Alice na kumfanya Larry atabasamu.
“nimekuambia mara nyingi. Na leo narudia tena kua sijaona mwanamke wa kuishi nae tofauti na wewe.
 Kama  si wewe, basi siwezi kuishi na mwanamke kabisa.” aliongea Larry na kumfaya Alice atabasamu.
“vipi kuhusu Sis. Deka?” aliuliza Alice kwakua alikua anamkumbuka vizuri.
“nimeshaachana nae.” alijibu Larry.
“vipi kuhusu mali zake alizokupa?” aliuliza tena Alice.
“alichonipa amenipa na hana haki ya kukichukua tena mpaka mimi nipende kumpa. Sababu kila alichonipa kwenye mapenzi yetu alitaka kiwe changu milele. Na wala hakiwezi kumfanya apungukiwe na utajiri alionao. Ila amini kua kwa sasa kila kitu kimeisha. Na nimefika pale nilipokua natamani kufika hapo awali..” aliongea Larry na kumfanya Alice asielewe alikua anamaanisha nini.
“umefika ulipokua unahitaji kufika?” aliuliza Alice.
“ndio.. Kama kumbukumbu zako zitakua nzuri kabisa, nadhani utakua unakumbuka sms niliyokutumia kwenye kipindi cha Radio kabla urafiki wetu haujakomaa. Kabla hujajua hisia zangu za mapenzi juu yako.” aliongea Larry na kumfaya Alice ajjaribu kuvuta kumbukumbu hiyo akilini mwake.alitumia sekunde kadhaa kushughulisha ubongo wake ili apate majibu sahihi. 
“natumaini umzima wa afya malikia wa moyo wangu. Naamini upo kazini muda huu lakini akili yangu inafanya kazi ya kuhakikisha nakua pamoja na wewe hasa kwenye usiku wa baridi ambao mashuka peke yake hayatoshi ila umbali wako ndio tatizo langu, na kupenda na nakuhitaji kwenye maisha yangu..bado hujawa, natamani ungenielewa japo kwa macho tu ili ujue kama nakupenda. Ipo siku utatambua kama nakupenda sana, … Larry.”
Sms hiyo ilisomwa hewani na baada ya kusomwa. Alice aliachia mziki hewani na kuichukua namba ya Larry na kumtumia sms.
“nani huyo uliyempa maneno mazito kama hayo?”
Sms hiyo ilimuinua Larry aliyekua amelala kitandani huku radio pembeni na simu yake mkononi na kufanya akae ili aisome vizuri.
“yupo msichana nineyempenda sana, sema hajui na mimi kwa sasa nasubiri muda ufike kwani ni mapema sana kumuambia.”
Alice aliyakumbuka maneno hayo na kumuangalia Larry. Alijua kua muda wa yeye kupendwa umeshafika. Alimfuata na kumkumbatia. Wote walijikuta wanalia na hakukua na haja ya kuongea chochote zaidi ya ishara zao kuonyesha kua wameunganisha mioyo yao pamoja.
ITAENDELEA ...........
 


ALICE THE SUPER STAR 41

Alikaribishwa atokeze mbele ya umati wa watu. Watu walishangilia sana na kila mmja akawa na shauku ya kujua Larry ataipokeaje zawadi ile ambayo kwa makadirio ya macho inaweza kufika bilioni 60.

Alifurahi sana na kushindwa kuongea mbele ya kadamnasi ya watu. Zaidi alimkumbatia tu Sis Deka na kumuambia kua yeye ndio malikia wake.

“sikuwahi hata siku moja kuwa utakuja kunifanyia makubwa kama haya mpenzi wangu. Yaani siamini kua kuna siku na mimi nitakuja kumiliki kampuni yangu mwenyewe. Ahsante sana mpenzi wangu.” aliongea Larry walipokua hotelini kwa ajili ya mapumziko  mafupi.

“huna haja ya kunishukuru mimi kwa kukupatia zawadi mpenzi wangu. Hayo ni moja ya majukumu yangu kama mpenzi wako wa dhati nikupendaye.” aliongea Sis. Deka na kmuangalia Larry ambaye muda wote alikua amejawa tu na tabasamu.

“sasa naweza sema kua naanza kuishi maisha ya ki super star.” aliongea Larry na kumfanya Sis. Deka atabasamu.

“larry... Wewe ni super star kuliko star yeyeote yule unayemjua. Kwangu mimi sioni wa kukufananisha naye.” aliongea Sis Deka na kucheka.

Walifurahia siku hiyo pamoja na kupigwa na upepo mwanana utokao katika fukwe za bahari iliyopo karibu kabisa na hoteli hiyo.



Waandishi wa habari walichapisha magazeti kila kukicha na kuuza sana kila walipokua wakiandika uhusiano huo kutoka kwa muigizaji wa nchini Tanzania na mwanamitindo tajiri Afrika kutoka nchini Afrika kusini.

Watanzania wengi waishio nchini Afrika kusini walifurahia sana kuona Mtanzania mwenzao akifanikiwa na kuwa mmoja wa matajiri chipukizi huko nchi za watu.

Miezi mitatu baadae, walirudi nchini Tanzania na kupokelewa na  matajiri mbali mbali wa serikalini na binafsi na kuandaliwa tafrija ndogo.

Kila mtu alitamani kufanya kazi nao kutokana na uzoefu wa biashara aliokua nao Deka.walifurahia sana ujio wao hapa nchini.

                                               *************************

Kampuni ya Alice the super star ilizidi kudidimia kwa kupunguza wafanyakazi kila kukicha kutokana na kutokua na fedha za kuendesha. Director ndio alikua msimamizi mkuu wa kampuni hiyo. Lakini kila kukicha ilizidi kumshinda. Aliandaa movie ambayo baada ya kutoka, haikufanya vizuri sokoni kwakua hakuwepo Alice wala Larry ndani yake.

Baada ya director kusikia ujio wa Larry nchini Tanzania, aliamua kuandika barua na kwenda nayo mpaka kwenye kampuni yao iliyopo huku nchini na kuomba kuoanan na Larry.

Siku tatu baadae alipigiwa simu na Larry na kumualika ofisini kwake.

“niambie ndugu yangu... Kwanza pole na kazi na majukumu uliyonayo.” aliongea Larry baada ya kumkaribisha Director na kusalimiana.

“nishapoa.. Ila nimekuja nina ombi katika kuinusuru kampuni ya Alice. Mpaka hivi sasa ninavyokuambia mimi imeshanishinda. Yaani nadaiwa na wafanyakazi na wengine wameacha bila kuchukua malipo yao. Hata nimejaribu kutoa movie, lakini imebuma na haijaleta faida ya kutosheleza..... Niambie Larry tunafanyaje?” aliongea Director na kumuangalia Larry amabaye allikua makini kumsikiliza.

“una story nzuri ambayo ipo tayari kwa kuchezeka filamu?” aliuliza Larry.

“story zipo.”

“niletee moja niipitie kisha nitakupa majibu.” aliongea Larry na kupeana mikono na Director.

Larry alichukua kitabu chake cha cheki na kumuandikia Director kiasi cha hela atakazochukua kwa ajili ya kuwalipa wafanyakazi mishahara yao.

“hakikisha hata wale walioacha kazi bila kuwalipa chochote inawafikia . Palipo pelea wewe nipe taarifa nitamalizia. Aliongea Larry baada ya kumkabidhi Director cheki ya shilingi milioni 200/=

“nashukuru sana.” aliondoka Director huku akiwa haamini kitu alichokifanya Larry. Tena kumuamini bila kuita mashahidi kwa hela nyingi kiasi kile.



Wafanyakzi walioacha kazi kutokana na malimbikizo ya mishahara yao, walistajabu sana baada ya kuona mishahara yao yote kuanzia nyuma imeingizwa kwenye account zao. Wafanyakazi waliokuwepo, walizidishiwa mishahara miwili mbele kama malipo ya uvumilivu wao.

“mkuu, wale walioacha kazi wameandika barua tena ya kujiunga. Tunawafanyaje watu hawa?” aliuliza Director.

“waruhusu waendelee na kazi.”

alijibu Larry na kumfanya Director kuwakubalia maombi yao ya kureje kazini. 



Baada ya kuchagua story nzuri, Larry alitangaza kambi baada ya kuwachagua washiriki ambao watakua pamoja katika filamu hiyo.



Waliingia location na matangazo juu ya filamu mpya ya Larry yalianza kuruka na watu wakaanza kuangalia ni kipya gani alichokuja nacho Larry.

Filamu hiyo iliyochukua masaa mawili na nusu. Iliwashika watu kutokana na story nyingi kufanana. Lakini hadithi aliyoitumia Larry ilikua ya kipekee.



Kutokan a na kujulikana kila mahali, aliweza kuuza fillamu hyo hususani nchini afrika kusini.

Watu walinunua filamu hiyo kama njugu na kuingiza mamilioni ya shilingi kuliko walivyofikiria.



“filamu imeingiza milioni 700. Ni zaidi ya malengo yetu tuliyojiwekea awali.” alionga Larry badaa ya mzunguko wa kawaida wa mauzo ya movie hiyo kkukamilika.



Waliiuza kwenye mtandao wa youtube na kupata feda zingine za ziada.

“sichukui hata shilingi mia katika mapato haya. Chansingi ni kuandaa movie nyingine na mapato yatakayobakia yakae kwa ajili ya marekebishoo ya jengo na akiba ya kampuni.” aliongea Larry baada ya kuwalipa watu migao yao na marupurupu nje ya mishahara anayowalipa.



Baada ya filamu ya pili kutoka. Sasa kampuni ya Alice the super Star ilirudi tena katika ramani. Ingawaje bado wazazi wa Alice hawakua tayari kushirikiana na Larry wakiamini kua yeye ndio sababu ya mtoto wao kuishi kwa mateso.

Larry hakujali, ila alihakikisha kampuni ya Alice the super Star inatengamaa tena.



Waliibua vipaji vipya ambayo vilifanya vizuri na kuaminika. Walijaribu kutoa movie moja bila ya kuwepo kwa Larry na badala yake alisimama nafasi ya Director Msaidizi.

Waliuza sana na kusifiwa kua kwa sasa kampuni yao inatoa filamu nzuri na ina wasanii wenye vipaji sana.



“nadhani kazi yangu nimeimaliza, ni muda mzuri wa kwenda south Africa na kuishi huko. “ aliongea Larry na kuwaaga wafanya kazi wa Alice.

“natumaini sitoiangusha kampuni. Na lolote litakalotufika, basi tutakupa taarifa.” aliongea Director na kumuaga Larry ambaye aliongozana na abiria wengine na kupanda ndege tayari kwa safari ya kuelekea nchini  afrika kkusini.

ITAENDELEA .................




ALICE THE SUPER STAR 40
Wakati anaongea Alice, alijisahau kua  anaingia barabara kubwa. Alishtuliwa na honi kali ambapo aligeuza shingo yake na kuangalia kushoto,alikuta gari imeshamfkia.
“MUNGU WANGU”
Ulikua mshangao wa watu walioshuhudia ajali hiyo ambayo ilimrusha Alice mita kadhaa na kumbilika kwenye lami huku damu zikimvuja.
Sauti ya ukelele wa Alice ulisikika kwenye sikio la Larry na ndio ikiwa mwisho wa kuisikia tena sauti hiyo-

                                                                                    ***********************************



Walimchukua Alice na kumuwahisha hospitalini. Huko alipelekwa kwenye chumba cha wagonjwa mahututi.

Taarifa za habari na magazeti yote yaliyotoka siku ya pili yake, yaliripoti ajalI mbaya iliyompata Alice.

Walliobahatika kutafuta taarifa kwenye blogs mbali mbali, walipata kuziona picha za Alice akiwa ICU. Walihuzunika sana kwa hali mbaya aliyokua nayo Alice, kupona ilikua ngumu sana kutokana na damu nyingi kumvuja

Madaktari walijitahidi usiku na mchana ili kuokoa maisha ya Alice.

“mama unatakiwa usaini ili tumfanyie upasuaji wa kichwa.” aliongea daktari baada ya kufika kwa mama yake Alice hospitalini hapo.

“jamani... Ataamka kweli?.”

Aluliliza mama yake Alice na kumshika daktari koti lake kwa uchungu.

“unatakiwa utulie mama na ufanye maamuzi hayo haraka... Tukichelewa tunaweza kumpoteza huyu.” aliongea  daktari na kumfanya mama yake Alice amuangalie baba yake Alice ambaye alichukua jukuumu la kusaini ili kuruhusu upasuaji huo kufanyika.



Madaktari bingwa kutoka kwenye hospitali kubwa hapa nchini ndio waliohusika katika kukamilisha zoezi hilo. Hatimaye Alice alifanyiwa operation na kutoleawa damu ambayo ilikua imeganda na kukaribia kabisa kugusa ubongo.

Kwa juhudi za madaktari, waliweza kufanikisha hilo zoezi na kupata majibu kamili.

“kwa jinsi hali ilivyokua mbaya. Niwe muwazi tu, kua Mgonjwa wetu hawezi kupata fahamu kwa kipindi hiki. Itamgharimu miezi nane mpaka mwaka. Atafumbua macho na baadae kuongea, lakini hatoweza kukumbuka chochote cha nyuma kwa kipindi hiki. Hivyo nadhani ni vyema mkamuuguzie tu nyumbani na kufuata dawa ambazo mtaelekezwa jinsi ya kumpatia.”

Aliongea Daktari baada ya kumaliza kazi yao iliyowagharimu siku tano.



Vyombo vya habari mbali mbali vya nje na ndani ya nchi, viliripoti hali mbaya ya Super star Alice na upotevu wa uwezo wake wa kumbu kumbu.

Kila mtu alimuombea Alice aweze kupona mapema kwa imani yake.

                                               *************************

Taarifa za ajali ya Alice iliyompata nje tu ya ofisi yake ndio iliyomfanya awahi kurudi mahali alipoenda. Lakini hakufanikiwa kumkuta Alice, kwani tayari alishakimbizwa hospitalini. Larry aliuliza ni wapi ambapo amepelejkwa Alice na yeye akaenda mpaka hospitalini.

Alishauriwa akae nje hadi hapo watakapo mruhusu aingie.

Baada ya kukaa kwenye benchi kwa muda usiopungua masaa mawili. Aliwaona wazazi wa Alice wakija mbio hospitalini.

Larry aliwasalimia lakini hawakuitikia zaidi ya kumpita na kumvaa daktari ambaye alikua anatoka katika chumba cha ICU.

“subirini pale ili tufanye huduma ya kwanza kwa mgunjwa.” aliongea daktari na kuwaacha pale pale.

“umefuata nini hapa?” aliuliza mama yake Alice huku analia baada ya kumuona Larry pale. Alimkwida kwa kujua huenda yeye ndio msababishaji wa mambo yote yale.

“kijana ni vyema uende... Hatukuhitaji hapa.” aliongea baba yake Alice na kumfanya Larry aondoke bila kubisha.

Siku tatu baadae Larry alipigiwa simu na Sis. Deka na kumuambia kua anamuhitaji aende South Africa.

Hakulaza damu, alichoamua ni kupanda ndege  mpaka huko Afrika kusini ambapo alipokelewa vizuri sna.

“nashukuru mpenzi wangu umekuja. Nahitaji uwe mkurugenzi katika kampuni yangu mpya ambayo natarija kuifungua this weak.” aliongea Sis. Deka na kumsogelea Larry na kuanza kumbusu busu.

“mbona ghafla hivi.. Na hukunishirikisha mpenzi wako jambo kubwa kama hili, kwanini lakini?” aliongea Larry huku akionyesha kutofurahia jambo hilo.

“this is sup rise for you, ndio maana nilitaka nilimalize kwanza ndio nikuambie. Kama nimekuudhi nisamehe mpenzi wangu.” aliongea Sis Deka na kumfanya Larry atabasamu.

Aliongozana nae mpaka chumbani ambapo walienda kuoga wote na baadae kulala pamoja.



Asubuhi ya siku inayofuata, walienda kufanya shopping ya nguvu na siku inayofuata ndio ilikua siku ya uzinduzi wa kampuni hiyo inayojihusisha na maswala ya uuzaji wa magari.

Uzinduzi huo ulioalika viongozi wengi wa serikali pamoja na wasanii mbali mbali kutoka nchi mbali mbali duniani kote, ndio ilikua gumzo kila mmoja alizungumzia ukubwa wa kampuni hiyo na show room yake ilivyojaa magari mengi na ya kisasa.

“leo ni siku muhimu sana kwangu na muhimu sana kwa mtu nimpendaye. Nimeamua kutumia nafasi hii kumtambulisha rasmi mpenzi wangu na hivi sasa tuna mipango kabambe ya kufunga ndoa. Nadhani hata yeye anaweza kua amesahau umuhimu wa siku ya leo. Ila ni siku yake ya kuzaliwa na nimetoa kampuni hii kama zawadi kwake. Ina maana kila kitu humu kimeandikwa kwa jina lake... Si mwingine, bali ni Mr. Larry Benson.”

aliongea Sis. Deka na kumfanya Larry asiamini kitu kilichotokea pale. Hakika ilikua sup rise kubwa sana kuliko sup rise yoyote ile ambayo ilishawahi kutokea katika maisha yake. Alikaribishwa atokeze mbele ya umati wa watu. Watu walishangilia sana na kila mmja akawa na shauku ya kujua Larry ataipokeaje zawadi ile ambayo kwa makadirio ya macho inaweza kufika bilioni 60.

ITAENDELEA.............




ALICE THE SUPER STAR 39
“ni mapenzi tu ndio yaliyoniifanya niweze kukopa hela zote hizo. Brayton alihitaji bilioni Tatu li akafanyie biashara huko Uingereza. Na alikua akizihitaji haraka na mimi sikua nazo kwa wakati huo. Ila kutokana na mahaba niliyokua nayo juu yake. Sikutaka aanguke wakati mimi ninaamiinika na naweza kuweka bond kampuni yangu na nikapewa hela hizo.Baada  ya kuchukua kiasi hicho cha fedha, alienda na kufanya vitu anavyovijua yeye. miezi sita baadae alinipigia simu na kunipa taarifa za kufa kwa biashara aliyokwenda kuifanya. Nilichanganyikiwa sana lakini nilijipa imani kua hayo ni matokeo ya biashara. Kuna faida na hasara.Kuanzia hapo tulisahau kabisa kua miaka mitano tuliyopewa haikuwa mingi. Fedha nilizozipata nilikua naendelea na ujenzi wa kampuni zangu na kuziboresha. Niliongeza wafanyakazi na kuagizia vifaa nya kisasa kutoka nchini marekani.Sikuweza kuhifadhi kiwango hicho cha fedha kwa miaka minne. Ndipo nilipopeleka milioni mia nne baada ya show yangu niliyoifanya nchini marekani. Ndio hivyo tena nilipopata hela nyingi kutoka kwenya show za barani ulaya ndipo nilipokutana na maumivu ya mapenzi kutoka kwako na kunifanya nifuje hela ikiwemo kuwalipa wafanyakazi wangu mishahara yao ya miezi minne. Sikuingiza hela tena zaidi ya kuitumia kwa fujo bila mpangilio.  Niliku tayari kufa na sikuona haja ya kuendesha kampuni tena kwani haikua na maana kwangu. Ila ujio wako na kunilipia hizo hela umenifanya nisahau kila kitu na kuyakabidhi maisha yangu kwako tena kwa mara nyingine. Naomba nikutamkie kwa ulimi wangu na kukiri kwa moyo wangu. Nakupenda sana Larry, nipokee...Please.”
Aliongea Alice na kumuangalia Larry ambaye hakujibu kitu zaidi ya kuniinamia tu.
“unaikumbuka siku uliyonikuta nimeumia na bandage nyingi huku nikiwa nasambaratisha picha yako..ni kitu gani niliongea?” aliuliza Larry baada ya kunyanyua uso wake juu.
:”nakumbuka, nakumbuka kila kitu.”Alijibu Alice.
basi huo ndio ukweli wangu kutoka moyoni. Hakuna mwanamke ambaye anaweza kuishi kwenye moyo wangu zaidi yako wewe. Kama si wewe basi mwanamke mwengine hana nafasi kwangu. Nitakua najiongopea sana kama nikisema sikupendi Alice. Huo ni uongo. Bado una kila kitu ambacho nahitaji mwanamke wa maisha yangu awe nacho. Ila nahitaji nikuombe kitu kama bado unanipenda na unahitaji niwe mume wako.” aliongea Larry na mwishoni alimuangalia Alice ambaye alikua mdogo kama pilitoni wakati huo.
“kwa jinsi ambavyo nimefarijika kusikia kua bado naishi kwenye moyo wako...niombe chochote nitakupa Larry.” aliongea Alice huku akimuangalia Larry bila kuwa na mashaka kwa kitu atakachokiomba.
“nahitaji uniache uhuru na kuwa karibu na Sis. Deka hata kama nikitangaza kua ndio mpenzi wangu kwa sasa, wewe ujue tu kua ninaigiza na si hali halisi. Kwani kuna hela nahitaji kuchota kutoka kwake. Ikiwemo hiyo niliyokulipia imetoka kwake pia. Sasa nahitaji kuchota kiasi kingine kwa ajili yetu hapo baadae. Nakuomba wivu uweke pembeni tucheze hiyo deal.” aliongea Larry na kumfanya Alice ajiinamie.
“mbona hizi tulizonazo zinatosha kabisa Larry. Tuache maigizo na tufanye kweli, nakuhitaji na nahitaji sana ndoa kwa wakaati huu. Wewe ndio mwanaume wangu wa maisha Larry.” aliongea Alice
“ndoa yetu mimi na wewe ni suprise kwa dunia kwa jinsi ambavyo watu hawafikirii hata kidogo kama mimi na wewe tuna mahusiano zaidi ya haya ya kawaida. Acha tuutumie muda huu kufanya makubwa ambayo yatalisimaisha jina letu bila kutetereka kutoka kwa mtu yeyote.” aliongea Larry.
“kuna kitu nahitaji kutoka kwako ili niamini kama kweli unanipenda.” aliongea Alice na kumuangalia Larry.
“najua unachokihitaji...na unafahamu kama ni mapema sana kukifanya. Ila kama ni muhimu kwako nipo tayari kufanya ili nikutoe wasi wasi.” aliongea Larry na kumfanya Alice atoe macho.
“unawezaje kujua mengi kutoka kwangu bila ya kukushirikisha?” aliuliza Alice na kumtazama Larry ambaye alikua
Anatabasamu.
“kipindi ambacho nimekukaribia niliweza kugundua mengi kutoka kwako hadi matamanio yako na kipi unapenda na vingapi hupendi... Ila ni vyema ukavuta subira ili kushinda matamanio yako. Jenga tena imani yako kwangu.” aliongea Larry na kumuangalia Alice.
“nahitaji niende na wewe kwenye eneo ambalo nadhani hata wewe utalifurahia.” aliongea Larry na kutoka na Alice na kuingia kwenye gari lake.
Walienda safari ambayo hata Alice hakuijua ni wapi anapelekwa. Gari iliingia kwenye hoteli moja iliyojificha maeneo ya ubungo na kuingia na Alice na kuchukua chumba. Alice hakua na hofu kwakua alikua na mtu anayemuamini. Waliingia wote chumbani na Larry akafunga mlango.
Larry  alikaa kitandani na kumkaribisha Alice ambaye wakati huo alikua amesimama na hakujua kua ni jambo gani lililomfanya Larry amuingize mule chumbani.
“unakumbuka nini ukikitazama hiki chumba cha hoteli?.” aliuliza Larry na kumtazama Alice ambaye wakati huo alikua amejawa na wasi wasi baada ya kukumbushwa dhumuni la kuingia chumbani.
“sikumbuki chochote.” aliongea Alice huku akiwa anatetemeka.
“unakumbuka siku uliyotolewa sana na kuniambie tuje tupumzike hapa?” alongea Larry na kumtazama Allice ambaye  naye alikua anamuangalia kwa wasi wasi.
“naomba tuondoke..sina amani ninapoendelea kukaa hapa.” aliongea Alice na kuangalia chini.
“unaonaje tukiitumia siku hii kuvunja ukaka na udada uliopo kati yangu na wewe na kufungua ukurasa mpya wa mapenzi kati yangu mimi na wewe?” aliongea Larry na kumfanya Alice atoe macho kama vile alikua hajasikia kitu kilichoongelewa.
“samahani..yaani unamaanisha?” aliuliza Alice huku akiwa hamuangalii Larry.
“kama huhitaji niambie kua sihitaji kuwa karibu na wewe wakati huu.. Kwani kipi ambacho hujakielewa nilipkuambia kua nahitaji tuzindue mapenzi yetu mimi na wewe?”  aliongea Larry kwa ukali kidogo na kumfanya Alice amuangalie kwa woga.
“sio kwamba sitaki...” alionga Alice na kukatishwa na Larry.
“ila... Najua kwanini unahitaji kuwa na mimi. Kama nimeweza kufanya makubwa kwa ajili ya mapenzi yetu, lakini wewe kwenye hili umekua mtata. Kwanini ?..na kama huniamini kwanini umeniambia kua unanipenda na haupo tayari kunipa hazina yako kwa muda huu. Nimegundua kua unahitaji kunitumia.. Siku njema.” aliongea Larry na kutaka kuondoka. Alice alimshika mkono, Larry aliputa na kuondoka.
Alice alijilaumu kwa kumkatalia Larry kushiriki nae uzinduzi wa penzi na kuanza kulia. Alitoka nje ya hoteli na kukodi Taksi mpaka ofisini kwa Larry.
“mbona toka mlipotoka pamoja hajarudi... Mtafute kwenye simu yake.” aliongea secretary wa Larry.
Alice alijaribu namba ya Larry lakini haikupatikana.
“nahisi namba niliyokua nayo haitumii tena. Au anatumia namba nyingine?” aliuliza Alice baada ya kuona kua hampati kwa mara kadhaa.
“mpigie kwa namba yake ya biashara.” aliongea secretary na kumpa Alice business card ya Larry.
Alice alipiga hiyo namba na kugundua kua iliua inaita. Alitoka pembeni kidogo ili huyo secretary asiyagundue maongezi yao.
“samahani kwa kile kilichotokea hotelini.” aliongea Alice baada ya Larry kuipokea simu yake.
“usijali... Ila unapokua na shida ya hela usisite kuniambia. Ni wazi kua tunaweza kuendesha mapenzi yetu kwa kutatua matatizo yako. Nimeishi bila kufanya mapenzi muda mrefu kwa kuishi na wanawake matajiri ambao wao hawana muda wa kuhudumia penzi zaidi ya kuwaza biashara zao muda wote. Ila kwako wewe nikajua ni muda mzuri wa kuwatumia hao kuchota hela huku wewe ukiwa ndio mtu pekee wa kushiriki na wewe katika kuyafurahia mapenzi kwa kula vya chumbani. Kumbe na wewe ni mmoja kati ya wenye nia ya kuchukua hela na kwenda kutumia na huyo uliyekua naye. Kila ulichokifanya hotelini kinafanana kabisa na kile ninachowafanyia hao wenzako....... Ningekua mroho ningefanya mapenzi na wewe mara nyingi kila unapopata matatizo na kulewa, lakini nilisubiri kauli yako tu kua na wewe unanipenda na ndipo nilipokuambia kua nahitaji tuzindue mapenzi yetu rasmi... Ila ulikua tayari kusema unanipenda huku ukiwa haupo tayari kunipa kila kilichopo kwenye mwili wako. ....nahisi sistahili kuushika mwili wako.” alilalamika Larry.
“naomba nisamehe Larry...hata mimi sikujua kama nitaweza kukukwaza kama hivyo. Please naomba unisamehe.” aliongea Alice huku akiwa amechanganyikiwa. Maana alihisi kujiharibia mwenyewe.
“hakuna ulichonikosea Alice...ila bado unaniona ni yule ambaye nimekua maamuma wa mapenzi yako kila siku.”aliongea Larry kwa hasira.
“upo wapi kwa sasa.”
Wakati anaongea Alice, alijisahau kua  anaingia barabara kubwa. Alishtuliwa na honi kali ambapo aligeuza shingo yake na kuangalia kushoto,alikuta gari imeshamfkia.
“MUNGU WANGU”
Ulikua mshangao wa watu walioshuhudia ajali hiyo ambayo ilimrusha Alice mita kadhaa na kumbilika kwenye lami huku damu zikimvuja.
Sauti ya ukelele wa Alice ulisikika kwenye sikio la Larry na ndio ikiwa mwisho wa kuisikia tena sauti hiyo.
ITAENDELEA KESHO.....


ALICE THE SUPER STAR 38
Hakuamini baada ya kuambiwa kua amelipa deni lake lote la bilioni 2.6 alizokua anadaiwa na kampuni hiyo.
“ni nani ambeye amenilipia hizi fedha?” aliuliza Alice huku akiwa na shauku ya kutaka kujua.
“LARRY BENSON ”
Alijibiwa hivyo na kumfanya Alice atoe macho baada ya kulisikia jina la Larry likihusika katika malipo ya deni lake kubwa lililomshinda kulipa.
Aliuchukua mkataba wake na kusaini. Aliondoka huku akiwa amejawa na furaha ya ajabu.
Alifika nyumbani na kujilaza kitandani, aliwaza maneno ya Larry walipokua wote Best Bite.
“kwanza nakuomba Radhi kwa yale yote niliyoyafanya kwako... Pili nimehuzunia sana na hatua uliyokua unataka kuichukua juu ya kampuni yako. Ila tambua kua kila nilichokifanya ni kwa faida yetu na nisingependa kuona nafeli katika hili.” aliongea Larry na kumfanya Alice amuangalie kwa jicho pembe.
“hakuna ulichowahi kufanya kwa faida yangu. Vyote unafanya kwa faida yako tena bila kujali nitadidimia kwa kiasi gani.... Najuta kukufahamu katika maisha yangu.”
Mawazo hayo yalimfanya achukue simu yake na kupiga namba ya Larry.
“namba ya simu unayopiga kwa sasa haipatikani...jaribu tena baadae.”
Alijaribu Alice mara kadhaa bila kupata majibu. Hakuweza kusubiri, alitoka mbio na kwenda kwenye gereji ya Larry.
“Kwa hivi sasa ameachana na shughuli hizi za gereji. Ametuachia sisi tuiendeshe na yeye ameamua kufanya shughuli zake na Sis.Deka.” aliongea mchoraji na kumfanya Alice ashtuke baada ya kusikia jina la Sis. Deka.
“wanashughulika na nini na ofisi zao zipo wapi?.” aliuliza Alice.
“hivi sasa Larry ni mwanamitindo mzuri na anatumika kutangaza nguo za Sis.Deka.” alijibu mchoraji.
“hawana uhusiano wowote wa kimapenzi?” aliuliza Alice na kuwafanya washangae na kutazamana.
“hawana.. Mana wanegeweka wazi na wasingeficha chochote.” aliongea mchoraji na kumfanya Akice atabasamu.
“unafahamu anapatikana wapi kama nikimuhitaji.”
Aliuliza Alice na kuelekezwa ofisi yao ilipo.
“ahsante,” aliitikia Alice na kuondoka.
Alifika kwenye ofisi aliyoelekezwa na kuingia mpaka reception.
“nina shida na Larry.”
Aliongea hivyo na moja kwa moja dada wa mapokezi alinyanyua mkonga wa simu na kumpigia Larry.
“boss, kuna mtu anahitaji kuonana nawewe....anaitwa Alice.......sawa Boss.”
Baada ya maongezi hao ya dada wa mapokezi alimuangalia Alice na kumpa maelekezo.
Alice alipandandisha ngazi na kwenda kwenye mlango alioelekezwa na kugonga hodi. Alikaribishwa na kufungua kitasa cha mlango huo taratibu.
Alikuta ofisi kubwa iliyorembwa vizuri huku kukiwa na nakshi za kushangaza.
 Kwenye kiti cha kuzunguka, alimuona Larry akiwa amejiachia kwenye kiti cha office hiyo kubwa.
Kama kawaida yake, nyuma kabisa kweye ukuta hakukosa picha. Safari hii kulikua na picha kubwa ya Sis. Deka.
“karibu.”
Alikaribisha Larry huku anatabasamu baada ya kuiona sura ya Alice ikiwa katika hali ya mshangao.
“najivunia kukufahamu Larry... Mpaka sasa siamini kua umeweza kufanya yote kwa ajili yangu... Na umejuaje kama mimi nilikopa na sijalipa mkopo wangu?” aliuliza Alice baada ya kutulia kwenye kiti na kumuangalia Larry ambaye muda wote alikua anatabasamu.
“siku hiyo tulikua wote hotelini baada ya kunipigia na kuniambia tuonane.........”
                                                                ***********************
“naomba tukutane Larry ABC hotel...nina tatizo kidogo nataka unisaidie kulitatua.” aliongea Alice baada tu ya Larry kuipokea simu yake.
‘sawa, nakuja muda huu.” aliongea Larry na Alice akakata simu.
Baada ya dakika ishirini, gari ya Larry ilipaki chini ya hoteli kwenye parking zake na kuwasiliana na Alice.
Alifika baada ya kuelekezwa na kumkuta Alice akiwa kama amechanganyikiwa.
“una nini Alice, niambie basi.” aliongea Larry baada ya kuona Alice akiwa ameitikia salamu yake kinyonge.
“sina amani nyumbani kwangu Larry. Brayton ananichanganya na kunifanya nikose raha katika maisha yangu ya mapenzi. Yaani mpaka nashindwa cha kufanya. Kuna wakati mwengine natamani hata kumuambia kama vipi tuachane ili kila mtu afanye mambo yake kulliko kuendelea kuwa maadui ndani ya nyumba moja.” alilalamika Alice.
“pole sana Alice, ila ni vyema ukatafuta tatizo lipo wapi kabla ya kulalamika na kuchukulia uzito swala hilo...inaweza kukusaidia kujua nini tatizo na vipi uaweza kulitatua tatizo hilo.” aliongea Larry na kumshika Alice kwenye bega kama njia ya kumfariji.
“samahani kidogo.”
Aliomba Alice baada ya kupigiwa simu na kwenda kuipokea pembeni.
Alice alikua ameweka bahasha ya A4 kwenye meza yao na ndani yake kulikua na karatasi kadhaa. Kwa maelezo ya Alice yalikua hayajitoshelezi kabisa na kiwango alichochanganyikiwa.
 Moja kwa moja Larry alihisi itakua zile karatasi zilizokuwepo kwenye mkataba ndio zilizomchanganya.
Aliamua kuzichukua baada ya kuona Alice alikua mbali na kuzipitia haraka haraka.
Larry alitoa macho baada ya kugundua ukweli uliopo kwenye karatasi ya juu tu.
                                                                        *************************
“hapo ndipo nilipogundua kua una deni kubwa ambalo linaweza kukufilisi. Ndio maana niligoma hapo awali kucheza filamu kwa sababu nilijua tu kama ingebuma basi ungeumia mara mbili na kunilaumu... Ilikuaje mpaka ukaamua kukopa hela zote zile ili hali wazazi wako wana hela za kutosha?”  aliuliza Larry na kumfanya Alice amuangalie kwa macho ya huruma.
“ni mapenzi tu ndio yaliyoniifanya niweze kukopa hela zote hizo. Brayton alihitaji bilioni Tatu li akafanyie biashara huko Uingereza. Na alikua akizihitaji haraka na mimi sikua nazo kwa wakati huo. Ila kutokana na mahaba niliyokua nayo juu yake. Sikutaka aanguke wakati mimi ninaamiinika na naweza kuweka bond kampuni yangu na nikapewa hela hizo.Baada  ya kuchukua kiasi hicho cha fedha, alienda na kufanya vitu anavyovijua yeye. miezi sita baadae alinipigia simu na kunipa taarifa za kufa kwa biashara aliyokwenda kuifanya. Nilichanganyikiwa sana lakini nilijipa imani kua hayo ni matokeo ya biashara. Kuna faida na hasara.Kuanzia hapo tulisahau kabisa kua miaka mitano tuliyopewa haikuwa mingi. Fedha nilizozipata nilikua naendelea na ujenzi wa kampuni zangu na kuziboresha. Niliongeza wafanyakazi na kuagizia vifaa nya kisasa kutoka nchini marekani.Sikuweza kuhifadhi kiwango hicho cha fedha kwa miaka minne. Ndipo nilipopeleka milioni mia nne baada ya show yangu niliyoifanya nchini marekani. Ndio hivyo tena nilipopata hela nyingi kutoka kwenya show za barani ulaya ndipo nilipokutana na maumivu ya mapenzi kutoka kwako na kunifanya nifuje hela ikiwemo kuwalipa wafanyakazi wangu mishahara yao ya miezi minne. Sikuingiza hela tena zaidi ya kuitumia kwa fujo bila mpangilio.  Niliku tayari kufa na sikuona haja ya kuendesha kampuni tena kwani haikua na maana kwangu. Ila ujio wako na kunilipia hizo hela umenifanya nisahau kila kitu na kuyakabidhi maisha yangu kwako tena kwa mara nyingine. Naomba nikutamkie kwa ulimi wangu na kukiri kwa moyo wangu. Nakupenda sana Larry, nipokee...Please.”
Aliongea Alice na kumuangalia Larry ambaye hakujibu kitu zaidi ya kuniinamia tu.
ITEANDELEA..................



ALICE THE SUPER STAR 37

“yule ni msichana mzuri, na hivi sasa wewe ni star mkubwa. Sasa akijipendekeza kwako unafikiri unaweza kukata wakati yeye ndio aliyekutoa?” aliuliza Deka na kumfanya Larry atabasamu.
“lakini...” aliongea Larry na kukatishwa kauli.
“sihitaji mjadala kwa hilo Larry.... Kama unanipenda basi utanisikiliza na kufuata ninayokuambia.”
Aliongea Deka na Larry akawa mpole. Hakutaka kumbishia msichana tajiri kama huyo kwa kuhofia kumkosa na kutofikia malengo yake juu ya msichana huyo aliyetokea kupendwa kupita maelezo.
                                                           ******************************
Siku zilipita na hatimaye tarehe za kuingia kambini kwa ajili ya movie mpya ya Alice zilifika. Alice aliamua kumtafuta Larry kwenye simu baada ya kuona kua asubuhi ya siku inayofuata ndio siku ya kuingia kambini.
“uko wapi Larry.” aliongea Alice baada ya Larry kutoonekana wala kutoa taarifa usiku huo. Kwani walikubaliana wakutane usiku na kuamkia kambini moja kwa moja.
“nipo Arusha huku Ice Hotel.” aliongea Larry
“oh my god. Arusha unafanya nini huko wakati  unajua kabisa kua kesho ndio siku ya kuingia kambini?” alillamika Alice.
“Usijali, nitafika hapo mapema kwa ndege.” aliongea Larry baada ya kuona Alice amebadilika.
“nakutegemea... Usiniangushe.” aliongea Alice na kukata simu.
Masaa yalisogea kwa kasi kubwa sana na kufikia muda wa kwenda kambini bila ya Larry kuonekana. Alice alichnganyikiwa na kumpigia simu Larry kwa mara kadhaa.
“namba unayopiga kwa sasa haipatiani...jaribu tena baadae.”
Hayo maneno yalijirudia mara nyingi kila alipojaribu kupiga simu. Alice alizidi kupagawa na hakujua kwanini Larry aliamua kumdanganya.
“tuondoke.... Labda atakuja location” aliongea director na kumuambia Alice aingie kwenye gari.
Walifika kambini na kukaa siku tatu bila ya Larry kutokea.
“vipi Alice, ...kama vipi tuvunje tu kambi. Maana naona muda unazidi kwenda na tunapoteza hela nyingi bila movie kuanza.” aliongea Director na kumshika Alice ambaye alikua analia na hajui kwanini Larry ameamua kumuumiza tena.
“sawa, unawaza  kuvunja kambi.” aliongea Alice na Director aliamua kuvunja kambi.
Moyo wa Alice ulizidi kuumia sana kila akikumbuka jinsi Larry alivyokua anamfanyia vitimbi. Hakupata jibu kamili ni kitu gani ambacho Larry alikua anawaza kichwani kwake mpaka anaamua kumfanyia hivyo. Muda mwingine aliwaza labda ni kisasi cha mapenzi baada ya kuteseka kwa muda mrefu. Lakini pale walikua wameungana kwa ajili ya kazi na si mapenzi, vipi aamue kutenda aliyoyatenda. Aliwaza sana na hakupata jibu.
                                                    *********************************
Ndani ya jiji la Paris kwenye hoeli moja ya nyota tano,Larry na Sis. Deka waliendelea kula nchhi na majani yake. Walikua kwenye swimming pool wakiogelea huku kila mmoja wao akiyafurahia mazingira katika kipiindi hicho kilichojulikana kama summer time.
Watu wengi wa jiji hilo walikua wanakitumia kipiindi cha kiangazi kwa kula raha kwwenye fukwe za bahari. Sis. Deka alitumia njia hiyo kuhakikisha Larry anakuwa nae muda wote.
“nashukuru sana mpenzi wangu kwa kuonyesha ni jinsi gani unapenda kuniona nikiwa na furaha. Unaonaje kama tukirudi Tanzania.” aliiongea Larry baada ya kuona siku zinazidi kwenda toka ahidiane na Alice kushiriki movie yake.
“kwanini sasa,.... Au hujapapenda hapa kesho twende New york.” aliongea Sis . Deka baada ya kuona Larry anahitaji kurudi nchini kwake.
“hapana, kuna kazi tu nahitaji kwenda kufanya. Pia nina mkutano na waandishi wa habari kuhusiana na mradi wangu niliofungua kwa ajili ya kuwasaidia watoto yatima.” aliongea Larry na kumfanya Sis. Deka atulie.
“sawa....ni wazo zuri mpenzi wangu.”
Aliongea Deka na kumbusu Larry.
“kwahiyo tunarudi lini Tanzania?” aliiongea Deka na kumuangalia usoni.
“wiki hii itkua bora zaidi.” aliongwea Larry na kumkazia macho Deka kuashiria kua alikua ana maanisha kile akisemacho.
Safari yao ya kurudi nchini Tanzania baada ya kutoka ughaibuni, ilikua ya siri na hakuna mtu ambaye alikua anajua kua Larry na Deka walikua wameenda wapi.
Walirudi ncini na kwenda kwenye hoteli ya Serena kwa ajili ya mapumziko.
“Kesho nitaenda nyumbani mpenzi wangu. Ila sitakawia, wikii hihii nitakuja kwa ajili yako mpenzi wangu. Kuna mambo naenda kuyaweka sawa.” aliongea Deka walipokua wamepumzika baada ya safari ndefu iliyowachosha.
“nikukumbuka sana mpenzi wangu...nakutakia safari njema.” aliongea Larry na wote wakacheka.
Walilala na kesho yake Sis. Deka alijiandaa na kuondoka South African kwa ndege ya saa tano Asubuhi.
Hapo ndipo Larry alipoamua kuwasha simu yake baada ya kuizima kwa kipindi chote cha safari yake ya kuelekea jijini Paris.
Sms nyingi ziliingia. Na alipoangalia, aligindua kua sms nyingi zilikua za Alice. Alirudi nyumbani kwake na kutulia. Alizisoma zile Sms na kuuzunika sana baada ya kugundua ni jinsi gani alikua amemuumiza Alice.
“i’m sorry Alice.”
Aliongea peke yake na kulegeza tai yake.
Aliwaza na kuwazua ni nini afanye, alipata wazo la kwenda kwenye kampuni ya Alice the Super star. Alifika hapo na kila mmoja alimshangaa hususani Director.
“ndio umefanya nini Larry, ni bora ungekataa mapema kushiriki hii filamu kuliko kutufanya sisi tupoteze muda bila kuandaa kitu chochote. Na unajua kua ni jinsi gani Alice anatoa mishahara kwa mwezi. Sasa anapokaa miezi sita bila kufanya kitu chochote na anatoa mishahara, atakua anapanda kiuchumi au anashuka?. Pia umemfanya asimuamini mtu yoyote kua anaweza kucheza vizuri zaidi yako. Umemuumiza sana Alice kwa kitendo ulichokifanya.” aliongea director baada ya kuingia ndani.
“yupo wapi kwa sasa?” aliongea Larry.
“yupo tu nyumbani kwao.. Ni mara chache sana ndio anakuja huku. Tena anampango wa kuiua kampuni yenyewe kwa sababu inamtia hasara.” aliongeza Director huku akisikitika kwa jinsi Alice alivyokua amechanganyikiwa.
“muite basi ili niongee nae, ila nisingependa ajue kama mimi nipo hapa muda huu.” aliongea Larry na director akachukua simu yake na kumpigia Alice.
Alipokea mama yake Alice na kumpa taarifa Director kua Alice alikua anaoga wakati huo.
“basi akimaliza muambie kua namuhitaji aje muda huu... Ni muhimu sana.” alisisitiza Director.
“sawa.” alijibu mama yake Alice na kukata simu.
Baada ya nusu saa, gari ya Alice iliingia pale na kushuka haraka na kwenda ofisini kwa Director wake. Alipofungua mlango, alimuona Larry yupo pale, alitaka kufunga mlango na kuondoka zake.
“usiondoke Alice, kuna mawili matatu nataka kungea na wewe.” aliongea Larry baada ya kugonganisha macho yake na Alice.
“i hate u Larry.” aliongea Alice kwa hasira.
“najua una kila sababu za kunichukia, ila ni vyema ujue ni kwanini imetokea kua vile. Hata mimi nimehuzunika sana ndio maana nahitaij sana mimi na wewe twende mahali tukaongee kiundani hili jambo.” aliongea Larry na Alice akakubali kutoka kwa shingo upande.
Safari iliishia Best bite na kukaa kwenye kona ambayo haikua na watu wengi.
“una jipya gani ambalo unaweza kuniambia nami nikakuamini Larry... Wewe ni muongo na mimi watu waongo sipendi kuwa nao karibu.” aliongea Alice na kumfanya Larry ajiinamie.
“kwanza nakuomba Radhi kwa yale yote niliyoyafanya kwako... Pili nimehuzunia sana na hatua uliyokua unataka kuichukua juu ya kampuni yako. Ila tambua kua kila nilichokifanya ni kwa faida yetu na nisingependa kuona nafeli katika hili.” aliongea Larry na kumfanya Alice amuangalie kwa jicho pembe.
“hakuna ulichowahi kufanya kwa faida yangu. Vyote unafanya kwa faida yako tena bila kujali nitadidimia kwa kiasi gani.... Najuta kukufahamu katika maisha yangu.”
Aliongea Alice na kunyayuka.
“nakuomba ukae tafadhali.” aliomba Larry lakini Alice hakuonyesha kua anahitaji kukaa tena.
“nakuomba usinitafute tena... Ishi maisha yako na yangu niachie mwenyewe.” aliongea Alice kwa hasira na kuondoka.
Akiwa njiani anaendesha, Alice alikua na mawazo sana.  Alimkumbuka Larry kuanzia siku ya kwanza anakutana nae mpaka hivi sasa ambapo ametokea kumchukia kuliko mtu yeyote yule katika maisha yake.
Alipigiwa simu na muakilishi wa kampuni ya DAIWAS ambayo Alice alikua ameingia nayo mkataba wa mikopo.
“tunakuomba ofisini muda huu... Ni muhimu tafadhali.” aliongea muwakilishi huyo na kumfanya Alice atoe macho kidogo.
“sawa.” alijibu Alice na kugeuza gari kuelekea huko alipopigiwa simu.
Alifika kwenye jengo la ofisi hiyo huku akitweta na kwenda moja kwa moja hadi ofisini kwa mkurugenzi na kuomba ruhusa ya kuingia.
“samahani Aliice kwa kukusumbua, ila ni vyema ukikamilisha kusaini hapa kwenye huu mkataba wa marejesho yako. Tumefaniikiwa kupokea kiasi cha fedha kilichotumwa katika kuhakikisha unalimaliza kabisa deni lako.” aliongea mkurugenzi huyo huku anatabasamu. Alice alibaki ametoa macho tu, kwani alikua anajua wamemuita ili wamuambie kua wameamua kumfilisi kwa kupitisha siku za malipo yake ya mkopo aliouchukua.
“samahani... Kama sijaelewa hivi. “ aliongea Alice huku akiwa haamini alichokisikia.
“nafahamu ni jinsi gani ulivyokua na pressure juu ya mali zako kutaifishwa. Ila kuna mtu amefika hapa na kukulipia madeni yako yote, huyo ndio ametuagiza uje u saini mwenyewe kwakua wewe ndio muhusika wa deni hilo.” aliongea mkurugenzi huyo na kumfanya Alice kuangalia huo mkataba wa marejesho.
Hakuamini baada ya kuambiwa kua amelipa deni lake lote la bilioni 2.6 alizokua anadaiwa na kampuni hiyo.
“ni nani ambeye amenilipia hizi fedha?” aliuliza Alice huku akiwa na shauku ya kutaka kujua.
“LARRY BENSON ”
Alijibiwa hivyo na kumfanya Alice atoe macho baada ya kulisikia jina la Larry likihusika katika malipo ya deni lake kubwa lililomshinda kulipa.
ITAENDELEA KESHO.....


ALICE THE SUPER STAR 36

Wakati wanaendelea na maongezi yao, simu ya Larry iliita na kumuomba Radhi Alice na kunyanyuka na kupiga hatua kadhaa na kwenda kuongea na hiyo simu aliyopigiwa.
“wewe nisubiri tu mpenzi wangu. Nina kikao na mtu muhimu kwa sasa. Nikimaliza tu nitakuwa hapo na tutaenda kuumaliza usiku wa leo tukiwa pamoja my love... I love you so much.”
Hayo ni maneno ambayo aliongea Larry kwenye simu alipokwenda pembeni.
Baada ya makubaliano yao, alirudi na kukaa kwenye kiti kwa ajili ya kuendelea na maongezi yao.
“toka ulipoondoka, hata movie yangu niliyo kuambia kua nataka kucheza, sikufanikiwa kuicheza tena kutokana na upweke niliokua nao juu yako.” aliongea Alice baada ya Larry kukaa pale.
“”wooh... Sasa hivi umepanga kuicheza lini?” aliuliza Larry huku anatabasamu.
“wewe tu Larry, now najisikia vizuri sana kuonana na wewe. Nahisi ni muda mzuri wa kucheza filamu kabla hujabanwa tena na muda.” aliongea Alice na kumuangalia Larry.
“nipe script.. Next month tutaingia location.” aliongea Larry na kumfanya Alice ashukuru sana.
Baada ya kuagana na kuondoka, Larry akiwa kwenye gari yake, alichukua sikmu yake na kuwasiliana na mtu wa upande wa pili.
“nipe dakika tano tu, nitakua hapo mpenzi wangu.” aliongea Larry na kuongeza spidi kwenye gari yake.
Alifika kwenye hoteli ya kimataifa yenye nyota tano na kumpigia simu mtu ambaye walikua muda wote wanawasiliana.
Alikuja mrembo kutokea nchini South Afrika ambaye ndio mwanadada tajiri anayesifika kuliko madada wote maarufu Afrika. Ni mwanamitindo pia ni mmiliki wa kamopuni ya Good Smell inayojiuhisisha na utengenezaji wa perfume za kiume.
Mbali na kiwanda hicho, lakini mitaji mingine ni mmiliki wa mtandao wa Smart ambao kwa sasa ndio umefika Tanzania.
Mwanadada huyo alikuja Tannzania siku hiyo na hapo ndipo alipofikia baada tu ya kutua katika uwanja wa mwalimu nyerere.
Anajulikana kwa jina la Sis. Deka. Lakini jina lake halisi ni DEKEA UKWU.
Ni Raia wa nchi mbili. Nigeria na Afrika kusini. Wazazi wake ni matajiri sana na walikutana huko south Afrika na kuamua kuishi huko.
Deka alikutana na Larry kwenye tamasha la wasani na wanamitindo lililofanyika katikati ya jiji la Johannesburg. Kila mmoja alifurahi kumuona mwenzake baada ya kusikia habari kutoka kwenye mitandao na media mbali mbali.
“nimefurahi sana kuonana na wewe Larry.”
Hayo ndio maneno ya ufunguzi baada ya kupata nafasi ya kupata chakula cha jioni wakiwa pamoja.
“hunishindi mimi Sis.Deka.”
Alijibu Larry na kuachia tabasamu.
Waliongea mengi sana ikiwemo kubadilishana mawasiliano.
Kabla Larry hajarudi kutoka huko, walitengeneza uhusiano wa kimapenzi na kurudi nchini akiwa na mahusiano na msichana huyo tajiri.
“nimekuweka sana eeh” aliongea Larry baada ya kukutana na mrembo huyo na kukumbatiana nae.
“kawaida tu..nimefarijika sana kukuona Larry.” alionga Sis.Deka na kuingia na Larry hotelini humo.
 Waliingia kwenye chumba alichokua Deka na kulala humo.
Asubuhi ya siku hiyo Larry na Deka walionekana wakifanya shopping kwenye duka kubwa la nguo maeneo ya mlimani city.
Waandishi wa habari hawakuachia tukio hilo lipite hivi hivi, waliwafuata baada tu ya kutoka humo ndani kabla hawajapanda gari.
“ni siku nyingi zimepita bila kujua una mahusiano na nani baada ya kuachana na Fabiana, je Sis. Deka ndio mrithi wa Fabiana?” swali hilo ndio swali lililolengwa na waandishi wengi wa habari waliwazonga eneo hilo.
“bado hatujaamua kuweka wazi kama sisi tuna mahusiano au laa, ila kwa sasa ni marafiki tu wa karibu.” aliongea Sis. Deka na kuingia kwenye gari. Jibu hilo lilimfanya Larry anyamaze bila kujibbu kitu chochote na kuingia kwenye gari hilo na kuondoka zao.
“unaonaje kama tukiyaweka wazi mahusiano yetu.”  aliongea Sis.Deja na kumkumbatia mpenzi wake kifuani
“sawa.. Ila ningependa watu wafahamu kama sisi wapenzi tukifikia hatua muhimu kama vile kuwatangazia umma kama tunahitaji kuoana... Au unasemaje?” alongea Larry na kumuangalia mpenzi wake.
“wazo zuri.. Ila waandishi wa habari wanasumbua sana huku kwenu... Unaonaje tukienda tu kwetu Afrika kusini na uwe unakuja huku kwa shughuli maalumu tu?” aliongea Deka na kumfanya Larry akohoe kidogo.
“kwa sasa nina project nyingi kiasi na watu wa nchi yangu.. Wiki mbili zijazo nitaingia Location kwa ajili ya kushiriki movie mpya ya Alice.” aliongea Larry na kumfanya Deka anyanyuke kifuani alipolala na kukaa.
“unasema?”
Aluliza Deka kwa kuhamaki huku akiwa kayatoa macho yake baada ya kusikia jina la Alice.
“kuna movie tunacheza na Alice,...vipi kwani?” aliuliza Larry kwa mshangao baada ya kuona mabadiliko ya Deka.
“toka awali nilipowaona kwenye ile filamu yenu, nilikua na mashaka na ukaribu wenu na nikahisi huenda ukawa na mahusiano nae ya kimapezi nje ya movie...ila nilipojua kua amegoma kuolewa na mtu ambaye alipendana nae kwa mika ingi, basi nikatkea kumchukia sana mwanamke huyo. Naweza sema kua hakuna msichana ambaye ninamchukia kama huyo.. Sihitaji hata uwe karibu naye tena.” aliongea Deka na kumuangalia Larry kwa macho makali kumaanisha kitu anachokisema.
“ila mimi nina uhakika kua kwa sasa hawezi kufanya chochote kwangu mimi.” aliongea Larry na kchezea mashavu ya mpenzi wake ambaye alikua bado amenuna.
“yule ni msichana mzuri, na hivi sasa wewe ni star mkubwa. Sasa akijipendekeza kwako unafikiri unaweza kukata wakati yeye ndio aliyekutoa?” aliuliza Deka na kumfanya Larry atabasamu.
“lakini...” aliongea Larry na kukatishwa kauli.
“sihitaji mjadala kwa hilo Larry.... Kama unanipenda basi utanisikiliza na kufuata ninayokuambia.”
Aliongea Deka na Larry akawa mpole. Hakutaka kumbishia msichana tajiri kama huyo kwa kuhofia kumkosa na kutofikia malengo yake juu ya msichana huyo aliyetokea kupendwa kupita maelezo.

ITAENDELEA................ 


ALICE THE SUPER STAR 35
“usijali mwanangu. Lakini hiyo sio dawa, pia sio njia nzuri kwa mtu maarufu kama wewe. Wewe ndio kioo chetu na watu wengi wanaishi kwa kukuiga. Wewe ni mfano kwa watu wote wanaotafuta njia ya mafanikio na vipi waishi ili wasishuke na waendelee kukubalika katika jamii. Sasa wewe umejivunjia heshima na kujipotezea mashabiki wengi kwa kutokua na subira. Unafikiri hata kama Larry akikukataa ndio itakua mwisho wa wewe kuwa star na kufikia malengo yako?. Sasa hao mashabiki wa kukufikisha unapo pataka unawakera. Watu wa media ambao wamekua karibu na wewe na kukutangaza unawatukana. Unafikiri kuna watu maarufu wangapi ambao wamepita na hivi sasa wanahangaika kurudi katika nafasi zao na watu wamewakataa na hawana nafasi tena!. Unafikiri watu wangapi ambao walikua wanapenda kuisikia sauti yako ukitangaza umewakosa kwa kitendo chako cha kuacha bila sababu maalumu?...badilika mwanangu na uwaite waandishi wa habari na uwaombe msamaha kwa kitendo ulichokifanya. Pia uombe msamaha kwa uongozi na urudi tena kwenye kazi yako ya utangazaji.... Rejesha heshima yako kwanza kabla hujamfikiria Larry katika maisha yako.” Aliongea mama yake Alice na kumyamazisha Alice ambaye alikua analia kwa kwikwi. “imenuima sana mama .” aliongea Alice huku analia. “najua,..ila unatakiwa kuwa na subira kabla ya kuamua kitu chochote...maana subira huokoa mambo mengi sana ikiwemo kukupa maamuzi sahihi. Kwani subira hukuchambulia kipi kibaya na kipi kizuri ukiendee na njia za kuiendea kwa usalama. Mgeuze Larry kama upepo uvumao kwenye msitu na hivi sasa hakuna miti, hakuna tena upepo na tafuta njia ya kuishi kwenye joto sawa na pindi ulipokua ukiishi kwenye upepo. Kubali kua mapenzi ni sawa na bahari, kuna kupwa na kujaa. Pia wewe ni mzuri hivyo usiatafute mapenzi, acha mapenzi yakutafute. Utayafurahia daima.” aliongea mama yake Alice maneno kuntu yaliyoingia sawia kwenye kichwa cha Alice. Jioni ya siku hiyo alikua na waandishi wa habari baada ya kuwasiliana nao na kuwaomba wapate pamoja chakula cha usiku. “nimejiona mjinga kwa kitendo nilichokifanya kwa kushindwa kuzuia hasira zangu na kutoa matusi hadharani. Hivyo nawaomba radhi waandishi wa habari na watanzania wenzangu wote waliokwazika na kitendo nilichokifanya. Nawaomba radhi kwa kosa hilo na makosa mengine ambayo kwangu mimi sikua nadhania kua ni makosa kufanya mbele ya jamii. Pia nimeandika barua kwa uongozi wa juu kwenye Radio niliyokua nafanya kazi kwa kuwataka wanirudishe tena kazini. Kama wakinikubalia basi nitaendelea tena kuwatangazia kipindi cha Amazing night.” aliongea Alice na kupigiwa makofi na waandishi wa habari waliofika pale. Taarifa za Alice kuomba radhi na kurudishwa tena kazini ziliwafanya mashabiki wake wengi waliokua wanipenda sauti ya Alice kufurahia sana. Hata Alice mwenyewe alijikuta amefurahi sana kwa jinsi ofisini kwao walivyompokea.
                            ***********************
Jina la Larry lilizidi kukua nchini Rwanda baada ya movie yao kuchukua tuzo za filamu nchini humo.pia alichukua tuzo kama kuigizaji bora wa kiume Afrika. Sasa hivi ameikua lulu. Pia amekua msanii ghali sana kwa kila muandaaji ambaye alikua anamuhitaji ilimlazimu kumlipa shilingi milioni moja kwa kila scene aliyocheza. Series ya My Queen iliyochezeka nchini kenya chini ya kampuni ya Enymore iliyop nchini Afrika kusini ndio iliyomuongezea kipato kwa kulipa kiasi cha dollar 195,000 kwa season moja ambayo ilikua na epsode kumi na nane. Series ya My Queen ilikua mwiho wa matatizo kwa kila aliyangalia hiyo series alikiri kua Larry ana uwezo wa ajabu sana kwenye uigizaji. Pia Lafudhi yake ya kiingereza ndio iliyowashangaza sana wafuatiliaji wa riwaya hiyo. Alikua na tone ya kuvutia sana na kila mtu alipend kwa jinsi alivyokua anaongea. Baada ya safari zake hizo kukamilika baada ya miezi mitano, alirudi nyumbani na kupokelewa kwa shangwe kubwa. Watanzania walijivunia sana kupata muigizaji mkali kama Larry. Alipofika aliitwa kwenye mkutano mkuu na waandishi wa habari kwa ajili ya kumuhoji safari yake kwa miezi yote na mafanikio yake kwa ujumla. “karibu sana Larry nchini... Umeipeperusha vyema bendera ya nchi yetu kwa kuwa muigizaji boa wa kiume Afrika. Hiyo ni heshima kubwa sana kwako na kwetu pia. Nini siri ya mafanikio yako?” aliuliza mmoja wa watangazaji walioalika kwenye mkutano huo. “kwanza kabisa ni kumshukuru Mungu kwa kuniwezesha kuwa na sauti ya kusikilizwa na kila mtu na kumfanya apende kitu ninachokifanya. Pia naweza kusema ni jitihada katika kukitumikia kipaji niilichojaaliwa ndio zimenifanya nifike hapa nilipo. Maana naamini kua watu wengi wana vipaji, lakini wanashindwa kufikia malengo yao kwa kutoviweka mkazo na kuamini kua watafanikiwa kupitia vipaji hivyo walivyojaaliwa.” Alijibu Larry huku kamera mbali mbali zikiendelea kummulika kama muheshimiwa fulani hivi hapa nchini. “ulikutana wapi na Alice mpaka mkafanikiwa kushirikiana na kutoa ile movie ambayo imetambulisha rasmi kipaji chako. Na vipi uliweza kuongea nae mpaka akakubali kuchukua story yako na kuitolea filamu?” aliuliza muandishi wa habari baada ya kupata nafasi. “hapo awali sikua a wazo la kuja kuigiza hata siku moja. Tena sikua na ndoto za kuja kua Star hata siku moja. Ingawaje nilikua mpenzi wa movie hususani ambazo anazitoa Alice. Kilichonisogeza kwa Alice ni mapenzi yangu kwake yeye. Nilikua chizi kila niisikiapo sauti ya Alice. Nilikua natamani sana japo kupata nafasi ya kumgusa lakini ilishindikana. Nilitumia muda mwingi bila kukata tamaa na kuamini kua siku moja nitamsogelea Alice na kuongea nae licha ya kua kuonana nae ni ngumu sana. Basi mwisho wa siku ndipo nipofanikiwa kukutana na Alice na kuanzisha urafiki nae na kunipa nafasi ya kuandika story. Sikutaka kucheza, ila director wake alisema kua ninapendeza sana kama nikicheza mwenyewe kutokana na uandishi wa story nlivyotaka mtu acheze mwenye vigezo kama vyangu. Basi ndio ikawa tiketi yangu ya mafanikio. Namuheshimu sana Alice na nipo tayari kufanya kazi yake tena bila malipo kama nilivyomuahidi hapo awali aliponihitaji wakati nina mikataba na watu wengine.” alongea Larry. Wakati huo Alice alikua kwenye Tv yake anaangalia mohojiano hayo. Hapo ndio Alice alipogundua kua Larry bado hana mawazo ya kutengana nae. Bado anathammini mchango wangu na anakumbuka nilipomtoa.” Aliongea Alice na kutabasamu. Usiku wa siku hiyo aliamua kumpigia simu na kumjulisha ni wapi wakutane. Larry alifika bila kukosa na kukutana na Alice ambaye hawakuonana kwa takribani miezi mitano. Muonekana wa Larry ulikua mzuri zaidi ya mwanzo kutokana na kujengeka kimazoezi na kuwa na mwenye mwili uliomvutia sana Alice. Muonekano wa Alice haukua mzuri kama awali. Alikonda na kenchi za kwenye shigo yake zilimpa muonekano usiovutia kama awali. “I miss you Alice.” aliongea Larry baada ya kukutana na Alice na kukumbatiana nae. “hunishindi mimi Larry.. Umeyabadilisha saa maisha yangu toka uliponiacha siku ile kwenye mataa na kunifanya nisiamini ulichokiongea mbele yangu.” aliiongea Alice. “nimezipata taarifa zako nikiwa huko nchini Rwanda, iliniuma sana na nilijua kabisa huenda mimi ndio niliikua chanzo cha wewe kufanya yote yale. Kwanini uliamua kua mlevi wa kupindukia na kuanza kuvaa vichupi hadharani?” aliuliza Larry. “yote ni kwa sababu yako Larry. Nlishindwa kujizuia baada ya kugundua kua hunipendi tena na haupo tayari hata kushiriki filamu yangu. Nikajua kua ndio nimeshakupoteza na siwezi kuwa na wewe tena karibu , wewe ni zaidi ya rafiki. Nimekupata kwa bahati mbaya kwenye maisha yangu, lakini hivi sasa nina kila sababu ya kukuweka karibu yangu kwa sababu umekua sehemu ya furaha yangu.” aliongea Alice na kumfanya Larry atabasamu. Wakati wanaendelea na maongezi yao, simu ya Larry iliita na kumuomba Radhi Alice na kunyanyuka na kupiga hatua kadhaa na kwenda kuongea na hiyo simu aliyopigiwa. “wewe nisubiri tu mpenzi wangu. Nina kikao na mtu muhimu kwa sasa. Nikimaliza tu nitakuwa hapo na tutaenda kuumaliza usiku wa leo tukiwa pamoja my love... I love you so much.” Hayo ni maneno ambayo aliongea Larry kwenye simu alipokwenda pembeni. ITAENDELEA...............

ALICE THE SUPER STAR 34


“isiwe kwa sababu yangu tu.... Mimi siwezi kukupenda tena wewe. Na hata nikikuambia nakupenda basi ujue haitotoka moyoni.”
Aliongea Larry na kumfanya Alice aumie moyoni mwake. Ukweli ni kwamba alifanya yote yale kwa ajili yake, ila leo ni wazi kua amechezea shilingi kwenye choo.
“tuachane na hayo...kuna kitu cha muhimu zaidi kilichonifanya nikuite Larry.” aliongea Alice na kumuangalia Larry ambaye alikua anatabasamu muda wote.
“ok..tel me.” aliongea Larry bila kukwepesha macho yake kwa Alice.
“nahitaji ushiriki kwenye movie yangu nyingine ambayo tutaingia location mwezi ujao.” aliongea Alice na kuskilizia majibu ya Larry.
“mwezi ujao...hapana, siwezi kukudannganya Alice. Kunazia mwezi huu mpaka mwezi wa tano nina project zatakazonibana sana na sitokua na muda wa kucheza movie yako.” aliongea Larry na kumfanya Alice ajisikie vibaya.
“kwanini Larry unakataa kucheza movie yangu?” aliuliza Alice huku sura yake ikionyesha wazi kuchukia.
“sijakataa Alice. Ila wewe mwenyewe fikiria kua wiki ijayo naenda Rwanda kucheza movie na Fabiana. Baada ya hapo kuna series naende kucheza kenya ambayo itanichikua miezi minne location. Sasa huo muda wa kucheza movie yako nitaupata wapi?... Wewe tafuta star mwengine ucheze nae.” aliongea Larry na kumuangalia Alice ambaye alionyesha hasira za wazi kwa Larry.
“wewe sio wa kunifanyia hivyo Larry... Wewe wa kuniambia umebanwa na shughuli za sanaa?...Larry.” alalamika Alice na kunyayuka.
“niliambiwa kua binaadamu hafadhiliki... Nilisema kua sio wote kwa sababu sikuwahi kuona mtu akikosa fadhila. Ila kwa sasa naamini huo msemo kwa kukushuhudia wewe ambaye sikuamini hata siku moja kama ungeweza kunikatalia jambo langu kwa yote niliyokufanyia Larry.okey, kwaheri.”
Aliongea Alice na kuondoka bila kusubiri jibu lolote kutoka kwa Larry.
                                                            *************************
Maisha ya Alice yalianza kubadilika na kuwa msichana ambaye anaandikwa kila siku kwenye magazeti kutokana na tabia yake ya kulewa kupita kiasi.
Ilikua mshanga kwa kila shabiki wa Alice. Alikua msichana ambaye hana scandle hata kidogo. Lakini pich zake akiwa amelewa huku akiwa amevaa nusu utupu ndio zilizomfanya watu washindwe kumuelewa .
“kipi kilichombadilisha jamani Alice, mbona alikua hana tabia hii wala hajawahi kuandikwa vibaya kwenye magazeti?” tabia yaki ilikua mada kila sehemu mitaani. Wengi walijua kua amelewa sifa kutokana na kiwangoo kikubwa cha hela alichokipata alipokua huko barani Ulaya.
Aliacha kazi kwenye kituo cha Radio kutokana na kutokua na muda wa kwenda kutangaza tena. Watu wengi walisikitika kwa uamuzi wa Alice wa kuacha kutangaza kutokana na kupenda sana kuisikia sauti yake.
“kwanini Alice umeamua kuacha kazi?” aliuliza mmoja wa waandishi wa habari waliojaana nje baada ya Alice kutngaza kua hiyo ni siku yake ya mwisho kutangaza na hatotangaza tena hicho kipindi.
“kila mtu ana ratiba zake katika aisha ya kawaida... Hivyo kwa sasa ratiba zangu zinanibana sana usiku na kipindi cha Amazing night ni cha usiku. Hivyo ili vitu vingine viende vizuri, lazima nipunguze vitu vingine.” aliongea Alice
“vipi kuhusu swala lako la kuwa mlevi kupindukia kwa kipindi hiki... Kipi kinachokupelekea kufanya hivyo?” aliuliza muandishi wa habari mwengine aliyechaguliwa kuongea.
“hayo ni maswala yangu binafsi sana. Si kila kitu nikifanyacho katika maisha yangu basi kiwe wazi kwa kila mtu.” aliongea Alice na kumruhusu muandishi wa habari mwengine aendelee kuuliza swali.
“lakini wewe ni kioo cha jamii, unachokifanya kuanzia tabia yako ya kilevi na vinguo vyako visivyokua na heshima vinaipeleka wapi jami yetu?” muandishi wa habari aliuliza swali lililomkera sana Alice.
“wewe mpumbavu una haki gani ya kuniuliza swali kama hilo!...hukufunzwa eeh?..mtoto wa malaya wee.”
Aliongea Alice kwa hasira na kuwafanya waandishi wa habari washangae.
“siku nyingine muwe na adabu mnapotaka kuhojiana na mimi...pumbavu zenu.” aliongea Alice na kuondoka.
Kesho yake asubuhi na mapema magazeti yote yalichapisha juu ya kitendo cha Alice cha kumtukana muandishi wa habari matusi ya nguoni.
Heshima ya Alice ilianza kushuka siku hadi siku. Hata wale watu waliompenda, walitokea kumchukia kwa taba yake mpya ya kujisikia.
“una nini mwanangu, umebadilika sana na vitendo unavyovitenda ni aibu kwa familia yetu.”
Aliongea mama yake Alice baada ya kumsubiri mtoto wake ambaye aliingia pale usiku wa manane akiwa amelewa chakari.
“mimi.nimechoka, acha niende nikalale”
Aliongea kilevi Alice na kumfanya mama yake atikise kichwa kwa huzuni.
“huo sio muenendo mzuri mwanangu... Sijapenda hata kidogo. Na kama utaendelea hivi, basi utatafuta pa kukaa na si hapa.” aliongea mama yake na na kumuangalia Alice ambaye alishalala pale pale sebuleni.
Alimuamsha na kumkokota hadi chumbani kwake na kumlaza.
Alice aliamka kivivu na kumkuta mama yake akiwa kwenye kiti akiwa anamsubiri aamke. Alihuzunika kidogo baada ya kuona mama yake ameshindwa kwenda kulala kwa ajili yake.
“nina mazungumzo na wewe...ni ya muhimu sana na nilikua nasubiri uwe na akili timamu ili tuongee.” aliongea mama yake Alice.
Alice alisogea na kumfuata mama yake huku kichwa chake kikiwa chini kwa aibu
“najua kuna kitu kinakusumbua, ni kipi hicho ambacho kinakufanya uwe hivi mwanangu?” aliuliza mama yake Alice baada ya ya Alice kukaa pale na kumsikiliza mama yake.
“ni mawazo tu mama na maumivu niliyonayo kwenye moyo wangu. Nampenda sana Larry na nimeikua tayari mpaka kuachana na Brayton kwa ajili yake. Lakini alichoniambia ndicho kilichonifanya nisione maana ya maisha tena. Amekataa hata kucheza filamu yangu kwa sababu ya mwanamke wake wa huko Rwanda. Amesahau kabisa kwamba mimi ndio niliyempa jina mpaka akatambulika na kila mtu. Sasa hivi amesaliti mkataba wangu na hata kucheza tu amekataa. Imeniuma sana mama.” aliongea Alice huku analia.
“usijali mwanangu. Lakini hiyo sio dawa, pia sio njia nzuri kwa mtu maarufu kama wewe. Wewe ndio kioo chetu na watu wengi wanaishi kwa kukuiga. Wewe ni mfano kwa watu wote wanaotafuta njia ya mafanikio na vipi waishi ili wasishuke na waendelee kukubalika katika jamii. Sasa wewe umejivunjia heshima na kujipotezea mashabiki wengi kwa kutokua na subira. Unafikiri hata kama Larry akikukataa ndio itakua mwisho wa wewe kuwa star na kufikia malengo yako?. Sasa hao mashabiki wa kukufikisha unapo pataka unawakera. Watu wa media ambao wamekua karibu na wewe na kukutangaza unawatukana. Unafikiri kuna watu maarufu wangapi ambao wamepita na hivi sasa wanahangaika kurudi katika nafasi zao na watu wamewakataa na hawana nafasi tena!. Unafikiri watu wangapi ambao walikua wanapenda kuisikia sauti yako ukitangaza umewakosa kwa kitendo chako cha kuacha bila sababu maalumu?...badilika mwanangu na uwaite waandishi wa habari na uwaombe msamaha kwa kitendo ulichokifanya. Pia uombe msamaha kwa uongozi na urudi tena kwenye kazi yako ya utangazaji.... Rejesha heshima yako kwanza kabla hujamfikiria Larry katika maisha yako.”
Aliongea mama yake Alice na kumyamazisha Alice ambaye alikua analia kwa kwikwi.

ITAENDELEA.............

ALICE THE SUPER STAR 33

“ndio mimi... Bado sijajua naongea na nani?” alisisitiza Larry kama hamfahamu aliyepiga simu.

“ok... Siku njema.”.

Aliongea Alice na kukata simu.

“Larry wa kujifanya haijui hata sauti yangu?”

Alibaki anajiuliza maswali bila kuyapatia majibu. Ilimshangaza sana na hakujua kwanini Larry aliamua kumfanyia hivyo.

Ili[pita wiki moja bila Alice kumpigia simu Lary. Hata hivyo hakuweza kupigiwa simu na Larry.

Tangu amefika, hakuenda kwa Brayon licha ya kupigiwa simu mara kadhaa iliyokua ikimtaka aende kuonana na mchumba wake.

Swala la Larry bado liilidumu kichwani kwake. Aliamua kwenda ofisini kwa Larry il waongee apate kufahamu nini Tatizo.

Alifika na kuwakuta wafanyakazi wa Larry wakiendelea na kazi huku kukiwa na mabadiliko makubwa sana. Kwanza Gereji ilikua kubwa sana na iliyopambwa vizuri.

Aliingia ndani na kupga hodi kwenye chumba cha mkurugenzi wa gereji hiyo.
“karibu”
Sauti ya Larry ilisikika baada ya Alice kugoonga hodi.
Alice aliingia na kukuta picha yake haipo kwenye ukuta wa ofisi ile. Na badala yake, alikuwepo msichana mwengine akiwa amejaa kwenye picha nyingine. Alice alipomuona yule msichana alishtuka sana, kwani alikua ni muigizaji hodari sana kutokea nchini Rwanda.
Alijikuta amepoteza dakika kadhaa kuashangaa mazingira hadi kukaa kwenye kiti wanachokalia wateja.
“karibu sana.”
Alikaribisha Larry.
“ahsante”
“unaweza kusema kitu kilichokuleta ofisini kwangu.” aliongea Larry na kumuangalia Alice bila kutabasamu kama alivyozoea.
“sikumbuki kama mimi na wewe tumeshawahi kugombana Larry.. Why umebadilika?” aliuliza Alice na kumuangalia Larry.
“ni kweli hatujawahi kugombana. Ila sihitaji tena uwepo wako karibu yangu. Kwani kufanya hivyo ni kukukoa wewe ili mume wako asiwe na mashaka na mimi. Ni hilo tu , wala usidhani kua kuna kitu kingine ambacho kimenifanya niwe hivyo.” aliongea Larry.
“bodp sijahalalishwa kuwa mke halali wa Brayton. Pia bado nina nafasi ya kubadili maamuzi na kuwa na mtu mwngine . Haya ni maisha na kila matu anahitaji ayafurahie kwa kiwango alichopangiwa kufurahia. Sasa kuishi nje ya furaha wakati una chaguo la kikataa karaha ni kujidhulumu mwenyewe.” aliongea Alice.
“ni vyema kama unafahamu hivyo . Hata mimi nimeamua kutoka kwenye uziio wa mateso ya kumpenda mtu ambaye siwezi kuwa nae, na hivi sasa nimeamua kuchagua njia iliyokua sahihi kwangu. Alice, kila nilipokua napiga hatua +kukukaribia, ndipo kiwango changu cha kujiumiza katika mmapenzi ndio kilikua kinazidi kupanda. Hata baada ya kuujua ukweli wako kuhusiana na na maisha yako. Bado nnilikua najipa moyo kuwa ipo siku utakua wangu kwa tukio lolotwe lile. Ndio maana hata uliponiambia niandika hadithi ya maovie inayohusiana na maisha yangu katika mapenzi, nimeandika ukweli kila kitu na baadae nikaandika matumaini yangu ya kuja kukupata kwa njia hiyo. Lakini kila kitu kilibadilika baada ya kuletewa kadi ya harusi. Kwa sasa naishi maisha tofauti na uliyokua umenizoea. Kwa sasa sina roho nzuri kama ile uliyonikuta nayo hapo awali. Na hata kama nikikuambia kua nakupenda hivi sasa, ni wazi nitakua nakudanganya. Nimeamua kulizika penzi la kweli ardhini na kuvaa mapenzi ya mwili na vile matamanio yangu yanavyonipeleka... Kiufupi kwa sasa unaweza kuniita play boy.”
Aliongea Larry na kumfanya Alice atumbue macho huku akiwa haamini kitu alichokua akiongea Larry.
“kwanini sasa umeamua kufanya hivyo... Wewe ni mbvulana mzuri. Unapaswa kua na msichana mzuri na kuishi naye. Kwani kwa saa unao uwezo wa kulilii familia na si hivyo unavyotaka kufanya Larry.” aliongea Alice huku akimuangalia Alice.
“majua unaweza kuongea chochote ambacho unajisikia kuongea kwangu mimi. Nilikua naridhika sana na kiwango cha fedha nilichokua nakipata pindi nilipokua gereji. nilikua napenda Sana kufurahi ndio maana kila muda uliniona nina tabasamu usoni mwangu, ila kwa  sasa nimezipata fedha lakini hulioni tabasamu tena. Si Larry yule uliyemzoea. Nimebadilika sana. Ila utambue tu kuwa sijabadilishwa na hela, bali nimebadilishwa na mapenzi. Kama nilikua masiikini na nikakataliwa na wewe. Hivi sasa nimepata fedha ndio nashuhudia kadi ya harusi ya mwanamke ninayempenda. Sasa unataka niweje yaani?... Yule niliyempenda ameondoka na mapenzi yangu yote. Sina nafasi tena moyoni mwangu ya kumuweka mwanamke mwengine.” aliongea Larry na kumfanya Alice awe hoi.
“ok... Ila mimi nimekuja kusuluhisha tofauti zetu kama kuna mtu amemkosea mwenzake. Maana sioni kama tuna ukaribu wa kutosha ambao unaweza kusema kuwa sisi bado ni marafiki. Nadhani unafahamu Larry kua mimi nafarijika kiasi gani ninapokua karibu na wewe.” aliongea Alice na kumfanya Larry amuangalie.
“wewe ni muongo na mbinafsi.. Unaijali furaha yako tu bila kujali mimi naumia kiasi gani. Kama ulikua hujui basi tambua leo. Kila ninapokua karibu na wewe, ndivyo kiwango cha maumivu kinavyokua kikubwa kila nikuonapo. Kila nisipokuona basi moyo wangu hua na amani na kila nikifikiria kua kwa sasa siwezi kuwa na wewe tena. Basi chuki hujijenga na kunifanya kua na hasira na wewe kwa muda wangu wote nilioupoteza kukupenda wewe.” aliongea Larry na kumuangalia Alice ambaye aliangalia chini.
“sina wazo la kuolewa kwa sasa. Nina mipango mingi sana ya kufanya ili kulisimamisha jina la kampuni pamoja na wewe. Natamani sana kufanya kazi zaidi na wewe. Kwani una nyota ya pekee Larry..” aliongea Alice na kumuangalia Larry.
“mimi sihitaj kufanya kazi tena na kampuni yako. Kwanza mimi ni msaliti na tayari nimeshavunja mkataba na kampuni kwa kuifaya kazi nje ya kampuni yako. Kwa hiyo kama mkataba ulivyosema kua kufanya kazi nje ya kampuni bila taarifa yoyote kutoka kwenye uongozi ni sawa na kujitoa mwenyewe.” aliongea Larry na kumfanya Alice amuangalie Larry.
“wewe ni tofauti sana na wasanii wangu wote. Ndio maana hata malioo ya ile movie niliamua tugawane bila kujali kua hukutoa chochote. Kwa hiyo hayo maswala ya kusaliti mkataba ni mambo madogo sana ambayo hata ukitaka kuwa huru kucheza nje ya kampuni mimi nitakuruhusu. Ila napenda sana kufanya kazi na wewe. Upo tofauti na wasanii wote niliowazoea..please.” aliongea Alice na kumfanya Larry amuangaliea Alice.
“ok...tupo pamoja.” aliongea Larry na kumpa mkono Alice.
Waliagana na Alice akatoka nje. Huko nje alikuta gari aina ya Altezza ikiwa imepaki nje na msichana mzuri akitoka kwenye gari hiyo. Alipomuangalia vizuri, aligundua kua alikua ni FABIANA.
Moyo ulimshtuka sana kwakua alikua anamfahamu Fabiana kama muigizaje mkali kutokea nchini Rwanda. Pia ile picha ya Larry aliyoiweka ilimtia mashaka kabla hajamuona Fabiana mwenyewe. Ila kwa sasa ndipo alarm ya hatari iligonga kichwani kwake na kumuambia kua kuna uwezekano Larry akawa na mahusiano na msichana huyo.
Aliinamisha sura yake chini na kuzitibua nywele zake ili asigindulike na kupishana na Fabiana bila kutambulika.
Aliingia kwenye gari lake na kuondoka. Alirudi nyumbani kwao na kumkuta Brayton akiwa sebuleni.
“nimekusubiri muda mrefu sana... Ulikua wapi Alice.” aliongea Brayton
“hiyo ndio salamu au?....mimi mfalme njozi nisime kua nimekuota kua kwa sasa unanisubiri?” aliongea Alice kwa ukali mpaka Brayton akabaki kwenye alama ya kuuliza.
“Alice ?.... Wewe wa kunijibu hivyo?” aliongea Brayton kwa hamaki.
“umeshaanza... Sema shida yako iliyokuleta na sio kuanza kuniwakia mpaka kwetu.” aliongea Alice na kusimama kwenye ngazi kama vile alikua anataka kwenda ndani na kumuacha mpenzi wake sebuleni.
“njoo basi kuna mambo mawili matatu nataka tuongee.” aliongea Braytona na kumfanya Alice arudi na kukaa kwenye sofa mbali kidogo na alipokaa Brayton.
“Hivi Alice, kuna kosa lolote ambalo nimekufanyia labda ambalo ukilikumbuka uanhisi hasira juu yangu?” aliuliza Brayton baada tu ya Alice kukaa.
“kwanini umeamua kuniuliza hivyo?” alijibu Alice kwa kuuliza swali na yeye.
“kiukweli sikusomi Alice. Maana toka upate matatizo siku ile ya ndoa yetu, imeuka ndio kama chanzo cha kuhitilafiana mimi na wewe. Sijui ratiba ya harusi ina semaje wala wazazi wako hawanipi maelezo yoyote juu ya mstakabali wa ndoa yetu. Mimi na wewe tuna miezi kibao hatujaonana wala huna muda wa kuonana na mimi. Kwanini Alice?” aliuliza Brayton na kumuangalia Alice.
“kwani wewe hujui ubize niliokua nao?... Toka nimerudi kutoka ziara yangu ya barani Ulaya,  nina muda gani mpaka sasa?.. Lini ulinipigia na kusema kua unaitaji kuonana na mimi zaidi ya siku ile niliyorudi tena nikiwa nimechoka na kuniambia nije kuchukua zawadi... Hayo huyaoni ila uinayaona yangu mimi ya kutokua na muda wa kuonana na mimi... Hiyo ni dalil tosha kua tumechokana.” aliongea Alice na kumfanya Brayton ashtuke baada ya kuisikia sauti ya Alice mwishoni mwa sentensi yake.
“unasemaje Alice?” aliuliza Brayton huku akiwa amehamaki
“kama ulivyosikia..sina muda wa kurudia.” aliongea Alice na kuondoka zake na kumuacha Brayton pale pale sebuleni.
Brayton alitoka na kwenda  kwa  mama yake Alice ambaye alikua nje akipunga upepo kwenye bustani.
“mimi naenda mama.” aliongea Brayton kinyonge.
“mboa haraka hivyo baba?” aliuliza mama yake Alice.
“sina tatizo lolote mama...ila nawahi tu kuna mahali naenda.” aliongea Brayton
“nakufahamu sana.... Ulivyokuja ulikua tofauti na ulivyo sasa. Au Alice amekuudhi?” aliuliza mama yake Alice na kumuangalia Brayton kwa macho malegevu.
“hapana mama.... Nitarudi jioni kwa sababu nina maongezi na nyinyi wazazi wangu.” aliongea Brayton na mama yake Alice alijua kutakua na tatizo tu.
“sawa.. Ila kama kuna hitilafu kati yenu...ni bora ungeniambia ili niweze kutatua mwanangu.” aliongea mama yake Alice
“kawaida tu mama... Baadae nitakuja tuongee tukiwa wote pamoja na baba.” aliongea Brayton na kuaga.
“sawa mwanangu... Baadae.”
Alongea mama yake Alice a Brayton akaondoka
                                                     **********************************************
Jioni ya siku hiyo Brayton alirudi kama alivyoahdi na kuwakuta wazazi wote wa alice wakiwa sebuleni. Alikaribishwa na kukaa karibu abisa na sofa alilokaa Alice ambaye wakati huo alikua anakula pop cone.
“nina maongezi machahe wazazi wangu nataka kuongea na nyinyi,.” aliongea Brayton baada ya kukaa dakika tatu. Wote walimgeukia na baba yake Alice alizima Tv.
“ongea mwanangu.. Tuna kusikiliza.” aliongea baba yake Alice.
“si dhani kama nina husika na kikao hiki.” aliongea Alice na kunyanyuka.
“hiki kikao kinuhusu mapenzi yetu.. Hivyo wewe ndio muhusika mkuu.” aliongea Brayton na kumfanya Alice arudi kukaa kwenye nafasi yake.
“kuna tatizo baba?” aliuliza mama yake Alice ambaye alikua anampenda sana Brayton.
“matatizo yapo.na ningependa leo tuyatafutie ufumbuzi wa kudumu.” aliongea Brayton na kuwafanya wazazi wake Alice wakae vizuri kumsikilliza.
“nimevumilia sana lakini leo naona ni vyema niongee duku duku langu lililonijaa moyoni. Mama mimi nampenda sana Alice nadhani hata nyinyi mnafahamu hilo. Tena upendo wangu ndio sababu iliyonifanya mpaka niwaite na kuwaambia kua ifanyike mipango ya ndoa. Ila tangu ndoa yetu ishindikane kufungika siku ile. Mwenzangu amebadillika sana. Amekua mkali,mjeuri na hta nikimwambia kitu chochote hataki kunisikiliza. Sasa ananiweka njia panda mwenzake na sijui mwenzangu kama bado yupo pamja na mimi au ndio keshaniacha.”
Aliongea Brayton na kumuangalia Alice.
“alice.... Tunahitaji majibu kutoka kwako, kuna nini kinaendelea kati yenu?” aliuliza baba yake Alice a kumuangalioa Alice ambaye hakua anaonyesha mshtuk wowote.
 
ITAENDELEA KESHO......   

 ALICE THE SUPER STAR 32
Vituo vyote vya habari hapa nchini na nje ya nchi, viliweka breaking news kuwa super star Alice aanguka kanisani wakati akifunga ndoa na kupoteza fahamu.

Walimchukua Allice na kumuwahisha kwenye hospitali iliyopo karibu na maeneo hayo ya kanisani.

Brayton  alibaki analia huku wazazi wa pande zote mbili wakimfariji na kumuondoa hofu.

Ilimchukua siku mbili Alice tangu apoteze fahamu na kurejewa na hali yake ya kawaida.

“pole sana Alice.” aliongea Brayton ambaye muda wote alikua pembeni yake.

Alice  aliangalia huku na huko na kuwaona watu wengi kiasi wakiwa wamejazana pale hospitalini.

“imekua vyema umepata fahamu muda huu. Kwani rais wa nchi yetu yupo njiani anakuja kukuangalia.” aliongea mama yake Alice na kumshika mkono mwanae.

“nini kimetokea mama... Mbona sielewi?” aliongea Alice huku akiyashangaa mazingira ya pale hospitalini.

“pole sana mwanangu kwa yote yaliyotokea. Ulipatwa na kitu kama mshtuko wakati tupo kanisani tukikamilisha ndoa yako. Kwa bahati mbaya ukazimia hata kabla hujamaliza kuapa mbele ya mchngaji na mashahidi tuliokuwepo. Ila usijali mwanangu, ukitulia tutafanya maandalizi ya harusi nyingine.” aliongea mama yake Alice na kumfanya Alice aelewe kipi kilichomlaza pale hospitalini.
Nusu saa baadae, rais aliwasili pale hospitalini na kutoa pole zake kwa Alice. Hiyo haikua mara ya kwanza kwa rais kumtembelea au kuwasiliana nae. Kwani rais mwenyewe alikubali kiwango alichonacho Alice na jinsi anavyoipeperusha bendera ya nchi kila kona ya dunia.
Baada ya wiki mbili kupita, wazqzi wa Alice waliamua kumuita mtoto wao na kumuambia kuwa analifikiriaje swala la kufunga ndoa nyingine baada ya ile ya mwanzo kuingiwa na hitilafu.
“kwa sasa akili yangu bado haijatulia mama. Pia ile tour yangu ya bara la ulaya inakaribia mapema tu mwezi ujao. So nahitaji muda mwingi wa maandalizi ikiwemo kufanya mazoezi ya kutosha ili nisijiharibie.” aliongea Alice na kumuangalia mama yake.
“mbona vipingamizi vimekua vingi mwanangu... Au humtaki tena Brayton. Maana hata kabla ya kutokea yale yaliyotokea. Ulikua huna furaha kama mtu ambaye alikua anafanya jambo kwa maamuzi yake....niambie ukweli mwanangu ili nijue.” aliongea mama yake Alice na kumuangalia mtoto wake.
“nampenda sana Brayton mama. Ila nahitaji muda zaidi wa kumsoma kwani mpaka hivi sasa bado hajatimiza vigezo vya kuwa mume bora kwangu.” aliongea Alice na kumfanya mama yake apigwe na butwaa.
“miaka mitano bado hujajua kama anakufaa au laa... Wewe sema ukweli, anakupiga?” aliuliza mama yake huku akiwa yupo makini na hakua kwenye masihara wakati anamuuliza hayo maswali Alice.
“hanipigi.” alijibu Alice kwa mkato.
“ana kunyanyasa?” aliuliza tena mama yake Alice.
“hapana mama ....ila niseme tu ukweli kua Brayton kabadilika sana. Sio kwamba amekua na idadi kubwa ya wasichana, ila ana wivu sana kiasi cha kwamba kunionea wivu mpaka na maprota wangu. Sasa nina wasi wasi nitakapofunga nae pingu za maisha. Anaweza kunizuia hata nisiimbe tena kitu ambacho mimi sitaweza kumtii. Hayo na mangine mengi ndio yanayonifanya nichelewe kujingiza kwenye ndoa.”
Aliongea Alice na kumfanya mama yake amuelewe kwanini alikua anasita sita kufunga ndoa na Brayton.

Watu takribani milioni 70 duniani kote ambao wame like page ya Alice the Super star walipata taarifa juu ya ziara kubwa ya Alice barani ulaya na kufanya show kwa miezi mitatu mfululizo kwenye nchi mbali mbal  barani humo.
Alipofika Uingereza, alipokelewa vizuri sana na show yake ilijaza watu kupita kiasi.  Mbali na kutumia uwanja wa Wembley. Bado kuna mashabiki wengine walikosa nafasi ya kuingia kwenye uwanja huo mkubwa wa kimataifa.
Baada ya show yake iliyotumia masaa manne jukwaani. Alirudi kwenye chumba chake cha mapumziko tayari kwa safari maandalizi ya safari yake kuelekea Ureno kwa ajili ya show kubwa jiini Lisbon
Asubuhi ya siku hiyo aliamua kwenda shopping kwa ajili ya kununua baadhi ya vitu ambavyo vilimvutia pale uingereza. Wakati yupo kwenye duka kubwa la nguo, kwa mbali alimuona mtu kama Larry akipita nje ya duka hilo. Aliamua kumfuata hadi alipokaribia kumfikia.
“LARRY!!!!!!!” 
Aliita Alice na kumfanya yule mtu ageuke nyuma. Alipoiona sura ya yule mtu. Ndio alipogundua kua hakua Larry, bali alimfananisha tu.
Alirudi kinyonge kwenye duka hilo na kuchukua mahitaji yake. Baada ya kumaliza kununua vitu alivyovitaka, alitoka na kwenda kupanga mizigo yake tayari kwa safari ya usiku.
Aliwasiliana na waandaaji wa nchini Ureno ambao walimkodishia ndege ya peke yake na kumfikisha nchini humo akitokea Uingereza.
Huko pia aliacha Historia na kupaza Jina la Alice kwa kufanya show ambayo iliwashangaza wengi sana waliohudhuria show yake.
Baada ya kuzunguka nchi zipatazo Kumi na sita, aliunganisha na Afrika kusini kwa ajii ya Show yake ya mwisho alizokua akizifanya kwa miezi mitatu mfululizo.
Ndani ya jiji la Johanisburg   alifanya show kwenye uwanja  mkubwa wa mpira uliokua katikati ya jiji hilo.
Baada ya mzunguko huo. Alirudi nchini Tanzania na kusubiriwa na maelfu ya watu waliokua wakimsubiri uwanja wa ndege wa mwalimu nyerere.
Alifika na kupanda gari la wazi huku waandishi wa habari wakihaha kwa kutamani kufanya nae mahojiano hapo hapo uwanja wa ndege.
Alifika nyumbani kwao na kujipumzisha.
Simu yake ilianza kuita baada ya kuweka tu Line. Jina lililosomeka ni Brayton
“heloo.” alipokea Alice
“niambie wangu.” aliongea Bayton kwa bashsha kubwa
“safi tu... Hata kunitafuta kwa Email umeshindwa?” aliongea Alice huku akiwa kenye hali ya kawaida.
“si unajua mpenzi wangu nilivyokua mvivu. Yaani huwezi amini nilikua nakuwaza muda wote na nilikua nasubiri tu urudi ili uje uchukue zawadi yako.” aliongea Brayton
“haya.... Nitakuja kuchukua hiyo zawadi.”
Aliongea Alice na kukata simu. Kabla hajaweka simu yake Pembeni, alikumbuka kumpigia Larry.
Alifurahi sana baada ya kusikia muito uliomjulisha kua namba aliyokua anaipigia iliku hewani.
“heloo”
Alipokea Larry baada ya simu yae Kuita muda mrefu
“woooh... Niambie Larry”
Aliongea Alice huku akiwa amejawa na furaha kupita kiasi ni muda mrefu sana hakuisikia sauti ya Larry.
“safi... Samahani nani mwenzangu, maana namba imekuja ngeni.” aliongea Larry na kumfanya Alice apigwe na butwaa. Hakuamini kua Larry anaweza kumuuliza swali kama hilo.
“lakini naongea na Larry?” aliuliza Alice.
“ndio mimi... Bado sijajua naongea na nani?” alisisitiza Larry kama hamfahamu aliyepiga simu.
“ok... Siku njema.”.
Aliongea Alice na kukata simu.
“Larry wa kujifanya haijui hata sauti yangu?”
Alibaki anajiuliza maswali bila kuyapatia majibu. Ilimshangaza sana na hakujua kwanini Larry aliamua kumfanyia hivyo.

ITAENDELEA.............

ALICE THE SUPER STAR  31
Upande mwengine alikuta maua na maputo makubwa na maandishi ya kumtakia ndoa njema. Chini kabisa alikuta saa ambayo Alice alimletea kama zawadi.
Hapo Alice alijua nini alichokimaanisha Larry. Alijua kua mpaka Larry amerudisha zawadi yake, basi hakuna kitakachoendelea kati yao.
“jianae basi mwanangu... Gari imeshafika kuja kukuchukua.”
Sauti ya mama yake ndio iliyomzindua kutoka kwenye mawazo aliyokua nayo juu ya maamuzi ya Larry juu yake.
Alijiandaa na kutoka nje. Alikuta magari aina ya Benz milango sita yakiwa matatu yaliyokua na rangi zinazofanana na kuingia kwenye benz moja illiyorembwa maalumu kwa ajili yake na safari ikaanza.
Walifika eneo la tukio na watu wote wakaanza kushangilia na maua mbali mbali wakimwagia Alice.
Aliungana na Brayton ambaye alivalia suti yake nyeusi safi iliyompendeza sana. Walishikana mikono na kusogea mbele ya kanisa huku mchungaji akiwa ameshika kitabu cha ibada ya ndoa kwa ajili ya kuipitisha ndoa hiyo.
Ilianza sala kwanza na baadae mchungaji aliwaamuru waangaliane.
Baada ya kuangaliana. Mchungaji aliongea machache pamoja na kuwahusia juu ya ugumu na wepesi wa maisha ya ndoa na kuwaambiia kua kwa sasa wanaenda kuwa mwili mmoja.
Kabla hajaendelea, mchungaji aliuliza swali ambalo lilimfanya kila mtu ageuze macho yake huku na huko kuangalia kama kuna mtu ataweza kuthubutu kuzuia.
“kuna mwenye pingamizi na ndoa hii?”
Hilo swali lilirudiwa mara tatu.
 Na hapo ndipo alipoingia mtu akitweta kwa nguvu huku shati alilovaa likiwa limejaa majasho na kuingia kanisani na kuwafanya watu wote wamuangalie.
“mimi napinga ndoa hii.”
Kauli hiyo iliwafanya watu wote waachame na kuguna. Alice hakuamini kua Larry ndio alikua amekuja kuisimamisha ndoa hiyo.
“una sababu za msingi za kupinga ndao hii isifungwe?” aliuliza mchungaji huku akiiweka miwani yake vizuri baada ya mtu huyo kuingia kanisani mule.
“hapo alipo Alice ni mjamzito wa miezi mitatu na mimi ndio muhusika wa mimba yake.”
Aliongea Larry na kufanya umati wote uliokusanyika pale kuguna na kushika kichwa. Mchungaji na Larry walibaki wametoa macho baada ya kupoka taarifa zile.
“una uthibitisho wowote?” aliulliza mchungaji.
“hata huyo bibi harusi ni uthibitisho  tosha. Muulizeni kama niyasemayo ni ya ukweli au naongopa.” aliongea Larry na kufanya watu wote kutulia na kumsikiliza Alice atasemaje.
“ni...ni kweli nina mimba yake.”
Sauti hiyo ndio iliyofanya watu wote kupiga kelele za kumtaka yesu ahimidiwe huku wengine wakimlaani shetani na kusema kuwa Alice ana mapepo.
Kofi kali kutoka kwa Brayton ndio lililomfanya Alice ashtuke na kujikuta yupo mbele ya mchungaji na yeye ndio anayetakiwa ajibu swali aliloulizwa.
“upo tayari kuolewa na Brayton Stephen?”
Hilo ndio swali ambalo alikutana nalo baada ya kugundua kua yale yote ya Larry kuingia na kuleta pingamizi yaliikua ni mawazo tu na haikua hali halisi.
Alitulia tu bila kufanya kitu chochote. Tukio hilo ndio lililofanya watu wote kutulia na kuangalia kwanini Alice alikua hajajibu swali hilo ambalo akikubali tu basi ndoa itakua imeshakamilika.
“upo tayari kuolewa na Brayton... Kuwa muwazi Alice kwani haya ndio maisha unayoyachagua kwa sasa.” alisisitiza mchungaji.
Bado   Alice alikua kama bubu na hakuweza kumuangalia mtu yeyote pale zaidi ya kuangalia chini.
                                                          *************************
Baada ya Larry kutoka nyumbani kwa kina Alice. Alirudi nyumbani kwake na kuanza kazi ya kubandua picha za Alice kwa mara nyingine. Safari hii hakutumia nguvu wala kuvunja fremu za picha. Alizitoa taratibu na kutoka nje na kuzichoma moto.
Alihakikisha kua hakuna kitu kitakachomfanya amkumbuke Alice tena nyumbani kwake.
Baada ya kumaliza usafi nyumbani kwake. Alihamia ofisini kwake. Aliiangalia sana picha hiyo waliyopiga pamoja. Hakuona sababu ya kuendelea kuiweka tena pale ofini kwake.
Aliitoa na kutoka nayo nje. Wafanya kazi wake walishangaa sana baada ya kuona picha ya Alice ikichomwa moto na Larry.
“kwanini bosi unaichoma moto?” aliuliza mchoraji ambayue ndio rafiki yake mkubwa kwa pale ofisini.
“it’s over now”
Aliiongea Larry na wote wakaelewa kwanini Larry aliamua kusema hivyo.
Hakuna mtu ambaye alikua hajui kuwa Alice alikua anaolewa siku hiyo.
“pole Larry... Kama umechagua moyo wa kupenda basi utampenda yule atakayekuja kukupeda tena hapo baadae.” aliongea mchoraji na kumshika bega Larry ambaye hakuwa na raha siku hiyo.
“sijisikii kufanya chochote kwa leo.. Naomba mtu yeyote akija kuniulizia mwambieni nimetoka.”
Aliongea Larry na kurudi ofisini kwake na kujifungia. Aliutazama ukuta ambao hapo awali ilikaa picha yake na Alice na kusikitika.
 Aliwaza siku ya kwanza kumuona Alice akiwa ameharbikiwa na gari na kupata nafasi ya kuonana nae.
Alifumba macho yake na hapo ndipo taswara ya denda katika scene ya mwisho alilopewa na Alice ilipokuja jkwa kasi na kusababisha mpaka machozi yaanze kumtiririka kwnye mashavu yake.
“why me?”
Alibaki kusema hivyo na kukaa kwenye kiti chake huku kichwa chake akiwa amekilaza kwenye meza huku machozi akiendelea kumwagika.
“good bye Alice.”
Moyo wake ulisema hivyo na kumsababishia angalau kupata nguvu na kuinuka. Alifuta machozi na kupiga moyo konde baada ya kuyakumbuka maneno ya mchoraji.
                                                  **********************************
Ukimya wa Alice uliwashangaza wengi kanisani na kuwatia hofu mpaka wazazi wake Alice. Hata Brayton mwenyewe hakujua kwanini Alice alishindwa kujibu kama amekubali kuolewa na yeye ama laa.
Wakati mchungaji akiendelea kumsisitiza Alice ajibu. Mara walianza kumuona Alice akishika kichwa kama vile alikua akisikia maumivu fulani.
Kabla hawajafanya lolote, walimuona Alice akianguka chini na kupoteza fahamu.
Vituo vyote vya habari hapa nchini na nje ya nchi, viliweka breaking news kuwa super star Alice aanguka kanisani wakati akifunga ndoa na kupoteza fahamu.
Walimchukua Allice na kumuwahisha kwenye hospitali iliyopo karibu na maeneo hayo ya kanisani.
Brayton  alibaki analia huku wazazi wa pande zote mbili wakimfariji na kumuondoa hofu.

ITAENDELEA .............



ALICE THE SUPER STAR 30 

Upande mwengine alikuta maua na maputo makubwa na maandishi ya kumtakia ndoa njema. Chini kabisa alikuta saa ambayo Alice alimletea kama zawadi.
Hapo Alice alijua nini alichokimaanisha Larry. Alijua kua mpaka Larry amerudisha zawadi yake, basi hakuna kitakachoendelea kati yao.
“jianae basi mwanangu... Gari imeshafika kuja kukuchukua.”
Sauti ya mama yake ndio iliyomzindua kutoka kwenye mawazo aliyokua nayo juu ya maamuzi ya Larry juu yake.
Alijiandaa na kutoka nje. Alikuta magari aina ya Benz milango sita yakiwa matatu yaliyokua na rangi zinazofanana na kuingia kwenye benz moja illiyorembwa maalumu kwa ajili yake na safari ikaanza.
Walifika eneo la tukio na watu wote wakaanza kushangilia na maua mbali mbali wakimwagia Alice.
Aliungana na Brayton ambaye alivalia suti yake nyeusi safi iliyompendeza sana. Walishikana mikono na kusogea mbele ya kanisa huku mchungaji akiwa ameshika kitabu cha ibada ya ndoa kwa ajili ya kuipitisha ndoa hiyo.
Ilianza sala kwanza na baadae mchungaji aliwaamuru waangaliane.
Baada ya kuangaliana. Mchungaji aliongea machache pamoja na kuwahusia juu ya ugumu na wepesi wa maisha ya ndoa na kuwaambiia kua kwa sasa wanaenda kuwa mwili mmoja.
Kabla hajaendelea, mchungaji aliuliza swali ambalo lilimfanya kila mtu ageuze macho yake huku na huko kuangalia kama kuna mtu ataweza kuthubutu kuzuia.
“kuna mwenye pingamizi na ndoa hii?”
Hilo swali lilirudiwa mara tatu.
 Na hapo ndipo alipoingia mtu akitweta kwa nguvu huku shati alilovaa likiwa limejaa majasho na kuingia kanisani na kuwafanya watu wote wamuangalie.
“mimi napinga ndoa hii.”
Kauli hiyo iliwafanya watu wote waachame na kuguna. Alice hakuamini kua Larry ndio alikua amekuja kuisimamisha ndoa hiyo.
“una sababu za msingi za kupinga ndao hii isifungwe?” aliuliza mchungaji huku akiiweka miwani yake vizuri baada ya mtu huyo kuingia kanisani mule.
“hapo alipo Alice ni mjamzito wa miezi mitatu na mimi ndio muhusika wa mimba yake.”
Aliongea Larry na kufanya umati wote uliokusanyika pale kuguna na kushika kichwa. Mchungaji na Larry walibaki wametoa macho baada ya kupoka taarifa zile.
“una uthibitisho wowote?” aliulliza mchungaji.
“hata huyo bibi harusi ni uthibitisho  tosha. Muulizeni kama niyasemayo ni ya ukweli au naongopa.” aliongea Larry na kufanya watu wote kutulia na kumsikiliza Alice atasemaje.
“ni...ni kweli nina mimba yake.”
Sauti hiyo ndio iliyofanya watu wote kupiga kelele za kumtaka yesu ahimidiwe huku wengine wakimlaani shetani na kusema kuwa Alice ana mapepo.
Kofi kali kutoka kwa Brayton ndio lililomfanya Alice ashtuke na kujikuta yupo mbele ya mchungaji na yeye ndio anayetakiwa ajibu swali aliloulizwa.
“upo tayari kuolewa na Brayton Stephen?”
Hilo ndio swali ambalo alikutana nalo baada ya kugundua kua yale yote ya Larry kuingia na kuleta pingamizi yaliikua ni mawazo tu na haikua hali halisi.
Alitulia tu bila kufanya kitu chochote. Tukio hilo ndio lililofanya watu wote kutulia na kuangalia kwanini Alice alikua hajajibu swali hilo ambalo akikubali tu basi ndoa itakua imeshakamilika.
“upo tayari kuolewa na Brayton... Kuwa muwazi Alice kwani haya ndio maisha unayoyachagua kwa sasa.” alisisitiza mchungaji.
Bado   Alice alikua kama bubu na hakuweza kumuangalia mtu yeyote pale zaidi ya kuangalia chini.
                                                          *************************
Baada ya Larry kutoka nyumbani kwa kina Alice. Alirudi nyumbani kwake na kuanza kazi ya kubandua picha za Alice kwa mara nyingine. Safari hii hakutumia nguvu wala kuvunja fremu za picha. Alizitoa taratibu na kutoka nje na kuzichoma moto.
Alihakikisha kua hakuna kitu kitakachomfanya amkumbuke Alice tena nyumbani kwake.
Baada ya kumaliza usafi nyumbani kwake. Alihamia ofisini kwake. Aliiangalia sana picha hiyo waliyopiga pamoja. Hakuona sababu ya kuendelea kuiweka tena pale ofini kwake.
Aliitoa na kutoka nayo nje. Wafanya kazi wake walishangaa sana baada ya kuona picha ya Alice ikichomwa moto na Larry.
“kwanini bosi unaichoma moto?” aliuliza mchoraji ambayue ndio rafiki yake mkubwa kwa pale ofisini.
“it’s over now”
Aliiongea Larry na wote wakaelewa kwanini Larry aliamua kusema hivyo.
Hakuna mtu ambaye alikua hajui kuwa Alice alikua anaolewa siku hiyo.
“pole Larry... Kama umechagua moyo wa kupenda basi utampenda yule atakayekuja kukupeda tena hapo baadae.” aliongea mchoraji na kumshika bega Larry ambaye hakuwa na raha siku hiyo.
“sijisikii kufanya chochote kwa leo.. Naomba mtu yeyote akija kuniulizia mwambieni nimetoka.”
Aliongea Larry na kurudi ofisini kwake na kujifungia. Aliutazama ukuta ambao hapo awali ilikaa picha yake na Alice na kusikitika.
 Aliwaza siku ya kwanza kumuona Alice akiwa ameharbikiwa na gari na kupata nafasi ya kuonana nae.
Alifumba macho yake na hapo ndipo taswara ya denda katika scene ya mwisho alilopewa na Alice ilipokuja jkwa kasi na kusababisha mpaka machozi yaanze kumtiririka kwnye mashavu yake.
“why me?”
Alibaki kusema hivyo na kukaa kwenye kiti chake huku kichwa chake akiwa amekilaza kwenye meza huku machozi akiendelea kumwagika.
“good bye Alice.”
Moyo wake ulisema hivyo na kumsababishia angalau kupata nguvu na kuinuka. Alifuta machozi na kupiga moyo konde baada ya kuyakumbuka maneno ya mchoraji.
                                                  **********************************
Ukimya wa Alice uliwashangaza wengi kanisani na kuwatia hofu mpaka wazazi wake Alice. Hata Brayton mwenyewe hakujua kwanini Alice alishindwa kujibu kama amekubali kuolewa na yeye ama laa.
Wakati mchungaji akiendelea kumsisitiza Alice ajibu. Mara walianza kumuona Alice akishika kichwa kama vile alikua akisikia maumivu fulani.
Kabla hawajafanya lolote, walimuona Alice akianguka chini na kupoteza fahamu.
Vituo vyote vya habari hapa nchini na nje ya nchi, viliweka breaking news kuwa super star Alice aanguka kanisani wakati akifunga ndoa na kupoteza fahamu.
Walimchukua Allice na kumuwahisha kwenye hospitali iliyopo karibu na maeneo hayo ya kanisani.
Brayton  alibaki analia huku wazazi wa pande zote mbili wakimfariji na kumuondoa hofu.
ITAENDELEA ............