Saturday, December 13, 2014


Umuhimu wa Jengo zuri kwenye utafutaji wa elimu unasaidia kumvutia mtoto na kumshawishi kupenda kuwepo eneo hilo na kujua kama mazingira ya shule nitofauti kabisa na mazingira mengine ya nyumbani kwao.
Kwa mtazamo wa haraka haraka jengo la shule kama hili lazima wakazi wa eneo hili au wanafunzi wa shule hii ni watu wa hali ya kawaida yaani ni Mikoani sio Mijini ndio kuna majengo kama haya kwa hiyo mtoto anajisikia hali ya kawaida kabisa na wala hawezi kuhisi kama hayo sio mazingira bora kabisa.




Uboreshaji wa majengo na ongezeko la madara ni dalili moja wapo ya kujua wakazi wa eneo hilo wana pokeaje swala zima la elimu.
Elimu ni ufunguo wa maisha inapofika shule ilipoanzishwa kulikua na darasa moja au matatu lakini baada ya mwaka ya kaongezwa mengine matatu bac ni wazi kuwa elimu imepokelewa vizuri eneo hilo na wakazi wanamsukuma na shauku kubwa juu ya elimu kwa vizazi vya eneo husika.




Umuhimu wa kumpa elimu mtoto wakike.
Ukimnufaisha binti kwa elimu umenufaisha jamii inayo kuzunguaka, zamani Tanzania yetu walisaminika sana watoto wa kiume ila kwasasa ni tofauti kabisa kwani familia nyingi au zote wanatambua nafasi za watoto wa kike kwenye swala zima la elimu.



watoto wadogo wa awali wakiwa nje ya jengo la darasa wafurahia.