MAKTABA KUU YA TAIFA.
Watanzania wengi tumekua wavivu sana wakujisomea na kusoma vitabu. Ukienda kwenye hilo jengo kwa kweli watu wanaosoma au kwenda kuazima vitabu ni wache sana.
Watanzania tuamke ifikie hatua kwenye kila Wilaya naVitongoji kuwe na Maktaba.
WATOTO WAKIJIFUNZA KUANDIKA
Watoto kama hawa wa kiongozwa vizuri watafika mbali sana kimtazamo maana mchezo wao umekua kalamu na karatasi.
Wazazi wakitanzani tujitahidi sana kuwaelekeza watoto wetu kwenye michezo yenye kufundisha na kuelimisha.
WANAFUNZI WA KIJISOMEA.
Wanafunzi wakike wakijisome kama tunavyo jua kwamba ukimuelimisha Mwanamke umeelimisha jamii nzima, kutoka na nafasi ya mwanamke na mtoto wakike kwenye jamii zetu za kiafrika au Tanzania, Watoto wakike ndio wako karibu na kila kitu katika familia husika.
WANAFUNZI WAKISOMA KWA MAKUNDI.
Umoja ni nguvu utengano ni udhaifu ifikie hatua wazazi tu wajengee watoto wetu tabia za kujumuika na wenzao kwaajili ya kubadilishana mambo mbali mbali wanayo kutana nayo mashuleni.
Wazazi wengi wanasomesha watoto shule za bording au shule za michepuo tofauti.