Thursday, April 23, 2015

 
RAMANI YA TANZANIA
 
Naipenda sana nchi yangu Tanzania yenye vivutio vingi sana, Tatizo ni moja tuu wananchi wengi wa Tanzania hatuna tabia za kufanya utalii wa ndani.
Ifikie hatua watanzania tuwena bashasha na hamu ya kutaka kujua mkoa gani kuna kivutio gani .
Japo kua vipato vyetu nividogo sana lakini tujitahidi kuijua nchi yetu.
Morogoro kuna mbuga ya wanyama Mikumi ila watanzani kwa mwaka wanaoenda pale ukifananisha na wageni Watanzania ni wachache sana.
 Hivyo hivyo Ngorongoro, Talangire, Saadani, Manyara nk.

Tanzania upande wa mashariki kuna bahari ya hindi lakini ukichunguza zaidi idadi ya wanaoweza kufanya michezo ya baharini  ni wachache sana, yote hiyo kutokana na kutokua na tabia ya kutumia vitu Mungu alivyo tujaalia.

Ifikia hatua watanzania tujitoe na tujifunze kutumia vitu Muumba alivyo tujaalia ndani ya Tanzani yetu.

 
BENDERA YA TANZANIA.